HUYU NDIO KIJANA MWAFRICA AMBAYE AMEBUNI SIMU YENYE UBORA SAWA NA ANDROIDS....SOMA ZIAD HAPA
Kila siku programu mbalimbali za simu za mkononi na kompyuta zimekuwa zikibuniwa. Kikubwa wabunifu hao wamekuwa wakitoka nchi zilizo nje ya bara la Afrika.
Lakini kijana kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo (DRC), Verone Mankou (27), amelipa bara la Afrika sura mpya
katika ulimwengu wa teknolojia za simu na kompyuta.
Naye amegundua programu zake za simu mithili ya
‘smartphone’ na kompyuta ndogo maarufu kwa jina la ‘tablet’Kwa mujibu wa
taarifa iliyochapishwa hivi karibuni na BBC, vifaa hivyo vinaendeshwa
kwa teknolojia ya Android ya Googles, na vinazalishwa chini ya kampuni
yake iitwayo VMK.
Akizungumza katika mkutano wa teknolojia
uliofanyika Afrika Kusini (Tech4Africa), Mankou alisema ubunifu huo ni
wa Waafrika kwani ndio wanaofahamu mahitaji ya bara lao.
"Apple ni kampuni kubwa Marekani, Samsung ni barani Asia, na tunataka VMK kuwa kampuni kubwa barani Afrika,"alisema.
Simu hiyo aliyoibuni ina kamera na skrini ya
ukubwa wa inchi 3.5 sawa na sentimita 8.9. Anasema kuna mipango ya
kuziuza simu hizo katika nchi kumi za Afrika Magharibi, pamoja na
Ubelgiji, Ufaransa na India.
Aidha, anasema anatarajia kuzindua uuzaji wa kompyuta za bei nafuu zaidi kwa wanafunzi mwaka ujao.
Kampuni ya VMK imesema kinyume na bidhaa nyingine
za awali za simu na kompyuta zilizosemekana kuwa za Afrika, bidhaa za
VMK hazifanani na bidhaa zozote za aina hiyo katika nchi nyingine.
Anasema kikubwa kilichomsukuma katika ubunifu huo
ni kutaka kuona watu wengi wanapata huduma za intaneti, hivyo
ilihitajika kupata kifaa kizuri kitakachopatikana kwa bei nzuri.
Mbio za kijana huyu zilianza mwaka 2006 ambapo
alikuwa akitoa huduma za intaneti, mwaka mmoja baada ya Steve Jobs
kutoa simu yake ya muundo wa iPhone, Mankou akaja na wazo la kubuni
alichokiita Big iPhone, akimaanisha kuja na bidhaa zake zenye ubora kama
Iphone).
Katika kufikia ndoto yake hiyo, alianza kwa kuunda
simu ya kisasa (Android) iliyokuwa inaitwa Elikia neno lenye maana ya
matumaini katika lugha ya Kilingala.
Aliendeleza mbio hizo mpaka Januari 2012 alipokuja na aina ndogo ya kompyuta (tablet) aliyoiita Way-C .
Huwezi kusema anatengeneza simu zenye ubora sawa na android maana android siyo simu, android ni operating system. Ila simu zake zinaonekana ziko poa anahitaji market
ReplyDelete