WALIMU WAMWAGA MACHOZI BAADA YA KUPANGIWA KUFUNDISHA KIGOMA....

Baadhi ya Walimu wapya waliopangiwa kufundisha shule za Msingi na Sekondari kwenye mkoa wa Kigoma, waliangua kilio muda mfupi kabla ya kupanda boti ya kusafiria kwenda kwenye shule walizopangiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma kwenye mwambao wa ziwa Tanganyika upande wa Kaskazini.
Kundi la kwanza la walimu 19 lilipangiwa kusafiri na boti ya Halmashauri ya wilaya ya Kigoma kwenye mwambao wa Ziwa Tanganyika lakini katika hali ya kushangaza baadhi ya walimu walianza kulia kama watoto wadogo wakihofia kwenda kwenye hizo shule kwa sababu mbalimbali kama vile kuhofia usalama wao na pia mazingira magumu ya kuishi.
Namkariri Mwalimu mmoja akiongea huku analia “kila mtu ana matatizo yake mimi siwezi nikaenda huko, tatizo sio maji…. alafu mimi nimebaki na mama tu, mzee wa miaka 60 yuko peke yake… bora nipelekwe sehemu nyingine”
Pamoja na kwamba ilikua ngumu, Mkurugenzi wa wilaya ya Kigoma Miriam Mbaga alifanikiwa kuwashawishi hao walimu na hatimae baada ya kama dakika 120 ndio wakakubali japo kwa shingo upande huku akisema, wengi walikua wanalia machozi na kujigaragaza, wengine walikua hawana mazoea ya kupita kwenye njia ya maji.
Kuna mwalimu anaitwa Wilfredias Cheche ambae amefanya kazi kwenye hayo mazingira magumu kwa miaka miwili, amesema “niko shule ya Msingi Kagunga Kigoma vijijini, mara ya kwanza nilifikiri mazingira ni magumu sana kama nilivyokua nasimuliwa, pamoja na kwamba ni mpakani na kuna vita ya hapa na pale… nawaondoa hofu walimu wenzangu, mazingira yanafaa kuishi”
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII

Copyright © 2013. ArtAfropixels Media.com - All Rights Reserved
Customized by: IT XPERTTZ ONE | Powered by: BS
Designed by: Tilabs