IRENE UWOYA NA DIAMOND WANASWA WAKIVUNJA AMRI YA SITA





Diamond na Uwoya, walifanya jitihada za hali ya juu kuuficha ukweli kuhusu uhusiano wao lakini ilipofika Machi 25, mwaka huu, walinaswa kwenye hoteli moja yenye hadhi ya nyota tano, iliyopo Mbezi Beach, Dar es Salaam.

 Ijumaa  lina ushahidi wa kutosha kutamka kwamba Diamond na Uwoya, walilala kwenye hoteli hiyo, chumba namba 208, waliingia saa 8:24 usiku kisha wakatoka kati ya saa 9:00 na saa 9:13 mchana.



Hii ni skendo  inayoweza kuweka rekodi ya kukaa kwenye vichwa vya watu kwa muda mrefu ujao, kwani Uwoya siyo tu kwamba ni mke wa mtu, bali pia ni juzijuzi tu alijidai amesahihisha makosa yake kisha akathibitisha kurudiana na mume wake, Hamad Ndikumana ‘Kataut’, baada ya kutengana kwa kitambo kirefu kidogo.


Skendo hiyo, inakuja na picha yenye mshtuko mkubwa kuhusu Diamond ‘Sukari ya Warembo’, kwani baada ya kumpitia Uwoya, ni dhahiri kwamba ndani ya Klabu ya Bongo Movie amebakiza wa kuhesabu, tena ni wale ambao mvuto wao ni wa kumulika kwa tochi, vinginevyo, vinara wote ameshadondoka nao dhambini.


Kwa kuanzia na Jacqueline Wolper, Wema Sepetu, Jokate Mwegelo, Aunt Ezekiel, Uwoya ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Bongo Movie Unit pamoja na warembo wengine kibao, ni wazi sasa mtandao wa ngono wa Diamond, unagusa karibu asilimia 97 ya mastaa wote wa filamu na muziki nchini...
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII

Copyright © 2013. ArtAfropixels Media.com - All Rights Reserved
Customized by: IT XPERTTZ ONE | Powered by: BS
Designed by: Tilabs