MAAJABU :MUME WA MTU ATIWA MBARONI KWA KOSA LA KUFANYA MAPENZI NA MBUZI MWENYE MIMBA NA KUHARIBU MIMBA YA MBUZI HUYO 

 
Marcel ambaye ni mume wa mtu, alifunguliwa kesi namba 29/2013 katika 
Mahakama ya Mwanzo ya Bashneti mkoani Babati kwa kosa la kuiingilia 
kimwili mifugo, kinyume na kifungu cha 325 kanuni ya adhabu, sura ya 16 
na kesi hiyo ilisomwa hivi karibuni.
Mshitakiwa aliwekewa dhamana 
lakini siku chache baadaye kesi ilipotakiwa kuendelea, hakuonekana na 
imebainika mahakamani hapo kuwa ametoroka.
Kesi hiyo ipo mbele ya 
Hakimu Julius Dagharo wa mahakama hiyo na aliyethibitisha mahakamani 
hapo kuwa mtuhumiwa ametoroka ni Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Bashneti, 
Omari Mwanditi.
Akizungumza mwishoni mwa wiki iliyopita, mmiliki wa 
mbuzi anayedaiwa kuingiliwa,  Clementina Masay alidai kuwa mtuhumiwa 
huyo amemsababishia hasara kwani mbuzi wake alikuwa na mimba lakini 
baada ya kitendo hicho, imeharibika.
Jamii ya wafugaji wa Kiiraq wa 
eneo hilo wamesikitishwa na kitendo cha mtuhumiwa kudaiwa kuiingilia 
mifugo yao kimwili mara kwa mara na wameahidi kumsaka hadi wamkamate.
Kamanda
 wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Babati, ACP Akili Mpwapwa amekiri 
kutokea kwa tukio hilo na ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa 
wakimuona mtuhumiwa huyo ili afikishwe mahakamani.
AMA kweli dunia imekwisha kwani mtu mmoja, Daniel Marcel (27), mkazi wa 
Kijiji cha Madunga, wilayani Babati, Manyara, amekamatwa na kufikishwa 
mahakamani kwa madai ya kufanya mapenzi
 
 TOA MAONI YAKO HAPA CHINI 
 
 
  
 
 
 
0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII