SOMA ALICHOKISEMA ZAMARADI MKETEMA BAADA YA DIAMOND KUMZAWADIA MZEE GURUMO GARI

Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Diamond Platnumz amemnunulia gari mzee ngurumo kama zawadi na heshima yake kwake kwa mzee huyo mkongwe wa muziki hapa nchini.
Mwanadada mtangazaji wa kipindi cha bongo movies nchini kinachooneshwa na kituo cha clouds TV Zamaradi Mketema ameshindwa kuzuia hisia zake baada ya tukio hilo la aina yake na kihistoria hapa nchini na kuamua kuandika yafuatayo kwa Msanii huyu anayefanya vizuri katika mziki wa kizazi kipya kwa sasa.
Kupitia mtandao, Zamaradi ameandika…
“Mtu anapofanya kitu kizuri hatuna budi kumpongeza... ameshafanya mazuri mengi, makubwa mengi na anaendelea kufanya mengi ya kuigwa.. amefanikiwa kuonesha taswira nyingine kabisa ya muziki wa bongo fleva.. ameweza kuprove kwamba kupitia MUZIKI tu unaweza kuishi na kufanya big things.. kiufupi amekuwa role model wa wasanii wengi wanaoanza muziki in EVERYTHING!!! As i said umefanya makubwa mengi lakini hili la kumnunulia Gari mzee Gurumo ambae alikuwa kwenye muziki kwa miaka 53 na hakufaidika chochote na muziki wake linaweza likaonekana la kawaida lkn kwa yeye KUWAZA na KUFANYA kitu cha aina hiyo anastahili pongezi kubwa sana kwakweli..ni moja kati ya makubwa na ya maana uliyoyafanya mwaka huu ...!!!! MUNGU atakubariki sana.. keep on shining @diamondplatnumz
Hongera sana Diamond.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII

Copyright © 2013. ArtAfropixels Media.com - All Rights Reserved
Customized by: IT XPERTTZ ONE | Powered by: BS
Designed by: Tilabs