HEBU ONA MAAJABU YA WANASAYANSI, WAMPANDIKIZA HUYU JAMAA PUA KWENYE PAJI LA USO
RAIA mmoja wa nchini China anayejulikana kwa jina moja la Xiaolian,
mwenye umri wa miaka 22, ametengenezewa pua nyingine na madaktari ambayo
sasa imewekwa kwenye paji lake la uso, baada ya ile ya asili kuharibika
katika ajali ya gari iliyomkumba Agosti, 2012. Madaktari wameitengeneza
pua hiyo kwa kutumia sehemu mbalimbali za mwili wa mtu huyo zikiwemo
sehemu za mbavu na ngozi yake. Operesheni hiyo imefanyika katika
hospitali moja huko Fuzhou, katika Jimbo la Fujian. Wataalam hao
wanatarajia kuihamisha pua hiyo na kuiweka sehemu ambapo pua yake ya
zamani ilipokuwa.
0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII