UWOYA MBARONI KWA WIZI WA SIMU...AFIKISHWA POLISI, SOMA HAPA
Na Waandishi Wetu
MSANII aliyewahi kutamba kisha kuporomoka kwa kasi katika tasnia ya filamu nchini Tanzania kwa sababu ya tabia zake chafu, Irene Uwoya, amefikishwa Kituo cha Polisi Msimbazi kwa wizi wa simu aina ya iPhone 5.
MAMBO yanaendelea kumwendea kombo mwigizaji huyo huku akiwa ameanza kuporomoka vibaya kwenye sanaa na kujikuta akiingia matatani kwa tuhuma za aibu.
HABARI ZA KIPOLISI
Kwa mujibu wa habari za kipolisi, mmiliki wa simu hiyo ni mwanamme aliyejulikana kwa jina la Mohammed Marjey, mkazi wa Dar.
Uwoya ambaye siku hizi anajitutumua kwa kuanzisha kipindi kwenye runinga moja ya Bongo baada ya kushindwa kwenye filamu, alidakwa na askari wa Kituo cha Polisi Msimbazi, Dar baada ya kusakwa usiku na mchana kwa kutumia kumbukumbu ya jalada la kesi namba MS/RB/8522/13 WIZI KUTOKA MAUNGONI.
MMILIKI AMWANIKA UWOYA
Akizungumza na Risasi Jumamosi juzi, Mohammed alisema simu hiyo aliinunua mwaka huu kwenye Duka la Grande Center jijini New York, Marekani alikokwenda kwa shughuli zake.Akasema Agosti 22, mwaka huu alirejea Bongo akiwa na simu hiyo ambayo ni toleo jipya la mwaka huu.
“Nilirejea hapa nchini nikiwa na simu hiyo. Tena unajua simu yenyewe ni ya kisasa, toleo la mwaka huu,” alisema Mohammed.Alisema Agosti 23, mwaka huu, akiwa kwenye gari katika Makutano ya Barabara ya Uhuru na Mtaa wa Nyamwezi, Kariakoo, Dar aliibiwa simu hiyo na mtu asiyemtambua.
“Nilikwenda Polisi Msimbazi kuandikisha maelezo na kupewa RB hiyo. Lakini nilitumia njia ya kitaalam kufuatilia, nikagundua simu yangu inatumiwa na mtu anayeitwa Peter, nikampigia simu kumwambia lakini hakuweka wazi aliipataje?
Mohammed alisema baada ya dakika kumi, alipigiwa simu na Uwoya na kumchimba mkwara kuhusu simu hiyo huku akisema ni yake yeye, jambo ambalo lilimshangaza jamaa huyo.
“Nilirudi Msimbazi na kuwaambia ndipo polisi wakaanza kazi ya kumsaka ili wamkamate. Leo (Alhamisi) amekamatwa akiwa na hiyo simu yangu,” alisema.
UWOYA AULIZWA ALIKOIPATA SIMU HIYO
Inadaiwa kuwa polisi walimuuliza Uwoya alikoipata simu hiyo ambapo alisema alipewa na jamaa yake wa Afrika Kusini huku mlalamikaji huyo akitoa risiti ya kununulia.
AONDOLEWA POLISI KWA MLANGO WA NYUMA
Baada ya kumaliza kuhojiwa kituoni hapo, Uwoya alitolewa kinyemela kwa mlango wa nyuma ili mapaparazi waliopiga kambi nje ya kituo hicho wasimfotoe.
MABALAA YA UWOYA
Makabrasha ya wasanii wa Tanzania ndani ya ofisi za Global Publishers zinamuonesha Uwoya akiwa anaporomoka kisanii siku hadi siku huku mabalaa mbalimbali yakimuandama ikiwa ni pamoja na fiamu zake kukosa soko madukani.
Kwa mujibu wa waandaaji wa filamu za Bongo, siku hizi hawamtumii msanii huyo kwa sababu kiwango chake cha kuigiza kimepotea hali inayowalazimisha kuachana naye au kumchezesha nafasi ndogo.
“Uwoya wa siku hizi si yule, nadhani kitendo cha kuanchana na Ndikumana (mumewe Hamad) kimempa mkosi, hana mvuto tena kama zamani. Mtu akitaka kutoa fillamu yake hawezi kumuweka Uwoya kwenye kava la mbele, ni majanga!
“Amekuwa akijitutumua ili aigize kama zamani, lakini wapi! Hana mvuto tena. Ilifika mahali anaomba kuigiza ili alipwe hata shilingi laki moja tu,” alisema muandaa filamu mmoja.
KUNASWA NA DIAMOND HOTELINI KUMEMDIDIMIZA
Habari zaidi zinasema kuwa ile skendo yake ya kunaswa hotelini akiwa na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kulichangia kumtumbukiza kwenye Top Ten ya Wasanii Wasio na Mvuto Bongo.
WADAU WASEMA ANA ‘LAZI’ YA MUME
Wengi waliozungumza na Risasi Jumamosi siku chache baada ya kunaswa hotelini walisema hawana sababu tena ya kuwa mashabiki wa msanii huyo kwani aliachana na mumewe na kutumbukia kwenye uhusiano na vijana wadogo jambo walilosema ni kama ‘lazi’ ya mumewe Ndikumana.
“Jamani huyu Uwoya si afadhali angeendelea kuwa na mume wake (Ndikumana), kamwacha sasa anatembea na vijana wadogo, akina Diamond. Lo! Mimi siwezi kuwa shabiki wake tena,” alisema Mwanahawa Mwarami ‘Mama Sumna’, mkazi wa Kijitonyama, Dar es Salaam.
WENGINE WAMNANGA
Septemba 10, mwaka huu, maeneo ya Mwenge, Dar, staa mmoja wa filamu za Bongo alimnanga Uwoya kwa kitendo chake cha kutangaza kuwakarabatia watu nyumba zao huku yeye akiwa hana nyumba aliyojenga.
“Unajua yule demu (Uwoya, eti amekuwa demu na si mke wa mtu au mama Krish) namshangaa sana, eti ana kipindi runingani anasema anakarabati nyumba za watu wasio na uwezo, halafu yeye mwenyewe hana nyumba, si upuuzi huo jamani?” alihoji staa huyo wa kiume.
Aliendelea kusema kuwa, Uwoya alishabugi siku nyingi hivyo anachofanya sasa ni kuhangaika pa kushika akiamini anaweza kurudia enzi zile za Oprah bila kujua kuwa, ‘bahati haiji mara mbili.’

0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII