HII NDIO AJALI ILIYOCHUKUA ROHO ZA WANAFUNZI WAWILI WA CBE DODOMA
Na John Banda, Dodoma
WANAFUNZI
 wawili wa chuo cha biashara  wamepoteza  CBE wamekufa papo hapo kwenye 
ajali baada ya kugonga tela la mizigo lililokwama barabarani baada ya 
kuhalibika.
Ajali
 hiyo ilitokea jana majira ya saa 1.00 usiku baada ya kugonga tela la 
lori la mizigo kwa nyuma wakati wanafunzi hao walipokuwa wakitokea 
kwenye mwaliko wa sherehe ya rafiki zao iliyofanyika katika kijiji cha 
ihumwa manispaa ya Dodoma.
Gazeti
 hili lilishuhudia msongamano mkubwa wa magari katika barabara hiyo 
iliyopo pembezoni mwa kambi ya jeshi ya Ihumwa kwa takribani saa zaidi 
ya tatu kabla ya polisi wa usalama barabarani kufika na kuongoza 
utaratibu wa kuondoka.
Kaimu
 kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Suzan Kaganda alisema chanzo cha ajali
 hiyo ni mwendo kasi wa wanafunzi hao wakati wakiendesha pikipiki hiyo 
 yenye namba za usajili T 420 CCN  waliokuwa wakukitokea barabara ya 
morogoro kuingia mjini.
Suzan
 aliwataja kuwa ni Ramadhan Lesso na Gerger Lwandala wanafunzi wa CBE  
na kwamba uzembe wa Dereva wa lori hilo lenye namba za usajili T 477 ABM
 na huku Tela lake ni T 838 AAZ aliyeliacha barabrani zaidi ya wiki bala
 kuweka alama yoyote huku matengenezo ya barabara hiyo yakiendelea katik
 eneo hilo.
Aliongeza
 kuwa miili ya marehemu hao iliyokuwa imehalibika vibaya kutokana na 
kufumuka fuvu la kichwa cha aliyekua dereva wa pikipiki hiyo  na ubongo 
kusambaa katika eneo hilo imehifadhiwa katika hospital ya mkoa.
Kwa picha za ajali hiyo bofya soma zaidi
lakini tunaomba radhi kwa picha hizo zinaleta usumbufu ukiziangalia

 Miili ya Marehemu Ramadhan Lesso na Gerge Lwandala inaonakana kabla ya kuondolewa katika kijiji cha Ihumwa barabara ya Morogoro Dodoma kabala ya kuondolewa na kuhifadhiwa katika chumba cha maiti hospital ya mkoa.

 Baadhi
 ya watu wakiisogeza miili ya Wanafunzi wa CBE Dodoma  walikufa kutokana
 na kuligonga tela la lori kwa nyuma kutokana na mwendo kasi huku lori 
hilo likiwa limetelekezwa zaidi ya wiki bila alama yoyote barabarani 
hapo.

 Baadhi
 ya asikari wa Jeshi la wananchi walionekana kujaribu kutoa msaada 
katika ajali hiyo iliyosababisha vifo vya wanafunzi wa chuo cha biashara
 CBE Dodoma.
 Asikari
 wa wasalama barabarani akisaidiana kupima upana wa barabara sehemu 
ilipotokea ajali hiyo ilihusisha pikipiki na lori la mizigo 
 

 
 

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII