TAZAMA PICHA ZA MAAFA YA KIMBUNGA KILICHOUA WATU ZAIDI YA 10,000 HUKO PHILIPINES
Wanajeshi
nchini Vietnam wakiwashusha wananchi kutoka kwenye lori wakati
wakiwahamishia katika maeneo salama kujikimga na kimbunga.
Wakazi wa Phu Yen, Vietnam, wakiandaa viroba vya mchanga kwa ajili ya kuweka juu ya paa za nyumba zao kujikinga na kimbunga.
Wafanyakazi
wa Shirika la Msalaba Mwekundu nchini Vietnam wakiweka mifuko ya
mchanga juu ya paa za nyumba ikiwa ni tahadhari dhidi ya kimbunga.
(PICHA ZOTE: EPA, AP NA REUTES)
-Red Cross wasema watu zaidi ya 1,200 wamepoteza maisha, 1,000 kati yao ni kutoka jiji la Tacloban, Leyte-Watu milioni nne waathirika na kimbunga hicho
-Miili yatapakaa mitaani, waokoaji walinganisha maafa hayo na Tsunami ya mwaka 2004
-Kimbunga hicho kinaelekea nchi za Vietnam na China
-Mamilioni wayahama makazi yao
-China na Vietnam wajipanga kukabiliana na kimbunga hicho
VIFO vilivyotokana na kimbunga kikali 'Haiyan' kilichoikumba nchi ya Philippines juzi Ijumaa vinadaiwa kufikia 10,000 imeelezwa.
Mpaka sasa taarifa kutoka Shirika la Msalaba Mwekundu zinasema watu 1,200 nchini Philippines wamepoteza maisha wakati wengi wakijeruhiwa lakini idadi hiyo inaweza kuongezeka.
1,000 kati ya waliopoteza maisha wanatoka jiji la Tacloban na kisiwa cha Leyte wakati 200 wakitokea Samar.
Kimbunga hicho kinatarajia kuikumba nchi ya Vietnam leo na baadaye China kwa mujibu wa taarifa za mamlaka ya hali ya hewa. Wananchi wa Vietnam na China wanachukua tahadhari kwa kujikinga na madhara yanayoweza kutokana na kimbunga hicho.
0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII