KIOJA CHA MWAKA, TAZAMA VIDEO HII YA MAITI ILIYOGOMA KUSAFIRISHWA





Jiji la Eldoret kaunti ya Uasin Gishu nchini Kenya leo lilishuhudia tukio la kushangaza baada ya maiti iliyokuwa inasafirishwa kwa maziko kukataa safari hiyo.

Kizaazaa kilizuka pale gari lililokuwa limelibeba jeneza lenye mwili wa marehemu kupata hitilafu na licha ya kubadilishwa gari jingine, nalo pia lilikataa kuwaka. 

Hapo ndipo marafiki na jamaa ya marehemu walipochukua fursa ya kuirai maiti hiyo ili ipate kufikishwa eneo la maziko. 

Baada ya maombi ya takribani saa moja kutoka kwa ndugu na jamaa wa marehemu kuiomba maiti hiyo ikubali kusafirishwa, hatimaye safari ilianza na kuacha maswali mengi yasiyo na majibu kwa mashuhuda wa tukio hilo.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII

Copyright © 2013. ArtAfropixels Media.com - All Rights Reserved
Customized by: IT XPERTTZ ONE | Powered by: BS
Designed by: Tilabs