TAZAMA PICHA ZA MAZISHI YA MWENYEKITI WA CCM ALIYEUAWA KWA MAWE NA WANANCHI HUKO MWANZA
Jeneza lenye mwili wa Clement Mabina likiwa mbele ya waombolezaji.
Waombolezaji wakiwa katika ibada ya kuuombea mwili wa marehemu Mabina kwenye uwanja wa Ngomeni-Kisesa, Mwanza.
Mbunge wa Sengerema (CCM), William Ngeleja akifuatilia ibada ya kuuombea mwili wa Mabina.
Ndugu na jamaa wakishiriki ibada ya kumuombea Mabina.
Jeneza lenye mwili wa Mabina likiwa eneo la kaburi.
...Likiingizwa kaburini.
Ndugu na jamaa wakiweka mashada ya maua katika kaburi la marehemu Clement Mabina.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria mazishi hayo eneo la Kanyamati, Kisesa mkoani Mwanza.
ALIYEWAHI kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Mwanza na
Diwani wa Kata ya Kisesa (CCM), Clement Mabina (56), amezikwa mchana huu
shambani kwake Kanyamati, Kisesa mkoani Mwanza. Mazishi hayo
yamehudhuriwa na Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, Waziri wa Nchi
Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wasira, viongozi wa
serikali, madhehebu ya dini, vyama vya siasa, wananchi na wakazi wa
Kisesa ambao wameungana na ndugu, jamaa na marafiki kumsindikiza
marehemu Mabina. Mazishi hayo yalitanguliwa na ibada iliyofanyika uwanja
wa Ngomeni-Kisesa, Mwanza
0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII