WEMA : "MARTIN KADINDA NDIO KILA KITU KWANGU"...DO YOU KNOW WHY?? SOMA HAPA
MSANII nyota wa filamu Bongo Wema Isack Sepetu amefunguka kwa kudai kuwa hawezi kuvunja urafiki na meneja wake Martin Kadinda kwa sababu kama kuna kitu chochote cha mafanikio nyuma yake yupo Kadinda.
Wema Sepetu ameuambia mtandao wa FilamCentral kuwa hana rafiki anayejua siri zake zaidi ya meneja huyo ambaye amekuwa akimuongoza vema.
“Kadinda
ndo kila kitu kwangu, hata akiondoka na kukaa mbali na mimi kwa muda
mrefu ninapokutana naye tu, nitamweleza kila kitu toka siku ya mwisho
tuliyoachana, hivyo inakuwa kama sijapoteana naye,yaani ni kama vile nipo naye
kila siku iendayo kwa Mungu,”anasema Wema.
Msanii huyu ameendelea kusema kwamba hata kampuni yake ya Endless
Fame film aliifungua kwa msaada wa Kadinda baada ya kumshauri kuwa kwa hadhi
yake anastahili kuwa na kampuni na aache kuigiza filamu za watu
wengine.
0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII