H.BABA : 'FILAMU ZINALIPA KULIKO MUZIKI'
BongoNewz
Mkali toka mwanza ambaye anatamba kwenye tasnia ya filamu na muziki hapa nchini Hamis Baba alias H.Baba amefunguka kwa kusema kuwa pamoja na yeye kuwa ni moja kati wa wasanii wachache wenye vipaji vingi, katika kazi zote ambazo amekuwa akishiriki sehemu ambayo angalau anaweza kuona fedha yake bila mizengwe ni filamu.
Kuhusiana na swala filamu lina lipa kuliko muziki H.Baba anasema”Kusema ukweli japo hatupati malipo ya kivile lakini katika filamu hakuna longo longo, uzuri wa filamu ni kwamba ukimaliza kazi yako ukikutana na msambazaji anakupatia fedha yako kulingana na mapato yako bila ya usumbufu, lakini katika muziki unasubiri hadi uuze kopi na haujui zinazalishwa ngapi?”.
Hitmaker wa “Mpenzi Bubu” ambaye sasa anatamba na ngoma yake aliyompa collabo Pasha kwa jina la “Thamani yetu” anazidi kufunguka kuwa toka aanze utayarishaji wa filamu hajawahi kusumbuka kuhusu malipo baada ya mapatano, msanii huyo anasema kuwa kulingana na hali iliyopo kwa wasanii wa muziki na filamu wanajikuta wakiwa na maisha ya kuazima magari na mavazi kwa sababu pato lao haliwafikii moja kwa moja.
H-BABA Katika Pozi.. |

0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII