Muuza magazeti aliyedaiwa kuuawa maandamano Chadema aibuka
BongoNewz
Muuzaji magazeti aliyedaiwa kuuawa wakati wa maandamano yaliyosababisha vurugu baina ya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na askari wa Jeshi la Polisi, maeneo ya Msamvu mjini Morogoro hivi karibuni, Kasim Mdangu ameeleza namna alivyonusurika katika vurugu hizo. Agosti 27, 2012 iliripotiwa na vyombo vya habari nchini kuwa askari wa jeshi hilo mkoani humo walifyatua risasi za moto na na mabomu ya machozi kwa wanachama na wafuasi wa CHADEMA waliokuwa wamejikusanya kwa ajili ya kuelekea kwenye mkutano wa chama chao na mtu mmoja aliyesemekana kuwa muuza magazeti aliuawa.
Akizungumza na NIPASHE katika eneo analouzia magazeti lilolopo Mtaa wa Msamvu Kata ya Mbuyuni mjini Morogoro, Mdangu alikanusha taarifa hizo na kusema aliyeuawa ni mbeba mizigo, Ali Zona. “Watu wengi walishangaa baada ya kuniona kwa sababu walipata taarifa kuwa nimeuawa katika vurugu za CHADEMA na Polisi, ukweli ni kwamba aliyeuawa ni ‘kuli’ (mbeba mizigo) Ali,” alisema Mdangu.
Alieleza kuwa Ali alikuwa akiishi mtaa wa Modeko ambao uko jirani na mtaa wao wa Msamvu na alikuwa akifanya kazi katika kituo cha magari ya mizigo yanayotoka mkoani Iringa kilichopo takriban mita 25 kutoka anapouzia magazeti. Alisema wakati wafuasi wa CHADEMA wakikimbizana na polisi, yeye alikuwa kwenye ofisi yake hiyo akiuza magazeti na baadaye marehemu (Ali) alifika kununua maji mahali hapo.
“Marehemu alikuja kununua maji maana kipindi hicho pia tulikuwa tukiuza maji hapa.
Gari la Polisi lilifika hapa likasimama, polisi wakaanza kutugombeza kwanini tumefanya mkusanyiko ilhali kulikuwa kumetolewa amri ya kutofanya maandamano, tukawaambia sisi hatukuwa na nia ya kuandamana wakaondoka,” alisema Mdangu.
Alisema “baada ya kuondoka baadhi ya watu waliokuwa hapa wakaanza kuwazomea…kwa jinsi lile gari la Polisi lilivyogeuka, nilijua kabisa kwamba kinachofuata ni kichapo nikaamua kukimbia.
Ali hakukimbia maana tulimwacha hapa akipitia magazeti. Ghafla tukasikia mlio kama wa risasi hivi, tuliporudi tukamkuta ameanguka chini na kichwa chake kilikuwa kimeharibika vibaya.” Mdangu alisema alishangaa kuona vyombo vya habari vikiripoti kuwa aliyefariki katika tukio hilo ni muuza magazeti katika eneo ambalo anauzia huku baadhi ya watu wakishtuka na wengine wakikutana naye wakiamua kumkimbia kwa sababu walipata taarifa kuwa ameuawa.
“Jambo hili limekuwa likinikosesha raha, lakini kaka yangu Mohamed amekuwa akinifariji na kunisihi niachane nalo kwa sababu mimi si wa kwanza kuzushia kifo,” alisema Mdangu. Awali ilielezwa kuwa wakati CHADEMA ikisisitiza kufanya maandamano kisha mkutano mkubwa wa hadhara, kuliibuka mvutano baina yake na polisi, kufuatia Kamanda wake, Faustine Shilogile kupiga marufuku mandamano hayo.
Kamanda Shilogile alieleza sababu za kuzuia maandamano hayo kuwa ni udogo wa barabara za Morogoro na kwamba ilikuwa ni siku ya kazi hivyo yanawezesha kusababisha usumbufu kwa wakazi wa mji huo. Wakati Shilogile akieleza kuzuia maandamano hayo, Mkuu wa Operesheni Sangara, Benson Kigaila, alisisitiza kuwa watafanya maandamano kwa kuwa waliskubaliana na Kamanda Shilogile kabla ya kuwageuka.
Ilielezwa kuwa Kamanda Shilogile alidai kuruhusu baiskeli na watu kutumia barabara kwa sababu ya mikutano ya Chadema itakuwa ni kuwanyima haki wananchi wengine, na hivyo wataruhusu watu wasiozidi 50 kupita kwa wakati mmoja pasipo kuwa na ishara ya kuonyesha kama wanaelekea katika maandamano.Katika tafrani hiyo, kijana Zona, ambaye alikuwa anasoma magazeti aliuawa wakati Polisi walipokuwa wakiwatawanya wafuasi wa CHADEMA.
Polisi walidaiwa kutumia risasi za moto na mabomu ya machozi kuwatawanya waandamanaji. Watu wengine waliojeruhiwa katika tafrani hiyo wameelezwa kuwa ni mwendesha baiskeli, Hashim Seif ambaye alijeruhiwa kwa kupigwa risasi mguuni akiwa anapita na baiskeli yake na kijana mwingine aliielezwa kuwa ni muuza matunda, Frank Valimba aliyejeruhiwa kwa kupigwa risasi tumboni.
Kwa mujibu wa ripoti ya uchunguzi wa madaktari wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, jeraha lililokutwa kwenye kichwa cha marehemu huyo lilitokana na kurushiwa kitu kizito. TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Kwa mujibu wa ripoti ya uchunguzi wa madaktari wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, jeraha lililokutwa kwenye kichwa cha marehemu huyo lilitokana na kurushiwa kitu kizito.
0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII