NACOPHA : "ARV SIO BANDIA, WANANCHI ENDELEE KUTUMIA".
BongoNewz
Ofisa Mtendaji wa Baraza la watu wanaoishi na virusi vya ukimwi (NACOPHA), Deogratius Rutawa |
Baraza
la watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi (NACOPHA), limewatoa wasiwasi
Wananchi kwamba dawa ya kupunguza makali ya Virusi vya Ukimwi
inayodaiwa kuwa ni bandia sio kweli.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Ofisa Mtendaji wa Baraza
hilo, Deogratius Rutatwa alisema dawa hiyo ni halisi bali siyo timilifu.
“Dawa hii siyo halali kwa matumizi ya tiba kamili kwa mujibu wa miongozo ya tiba iliyotolewa na Wizara ya Afya” alisema. Kwa
mujibu wa maelezo yake, dawa hiyo ambayo inadaiwa kuwa bandia ina
kiambatanisho kimoja tu, wakati tiba kamili inaviambatanisho vitatu.
Hivyo,
aliwasili watumiaji wa dawa halali yenye viambatanisho vitatu kuendelea
kuzitumia kwani wakiacha wanaweza kupata madhara zaidi.Alitumia
fursa hiyo kuwaomba madaktari wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha watumiaji
ambao wamepata dawa hizo (zinazodaiwa kuwa feki) wanazirudisha kwenye
vituo vyao kwa lengo la kupatiwa dawa halali.
Aidha,
alisema Serikali nayo itoe ufafanuzi kwa Wananchi ili wafahamu ni
madhara kiasi gani yaliyosababishwa na utumiaji wa dawa ambayo siyo
timilifu.
0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII