CHALZ BABA: 'GAZETI LA AMANI LIMENICHAFUA'

BongoNewz
Msanii nguli wa muziki wa dansi nchini, Chalz Baba amesema kuwa gazeti la Amani limemchafua kwa kuandika kuwa anataka kumuoa Lulu na tayari ameshaenda kwa mzee Michael kujitambulisha. Anasema habari hizo sio za kweli ni za kumchafua tu, aliyasema hayo alipokuwa akiongea na MPEKUZI

Alipoulizwa ni hatua gani atachukua baada ya kuona habari hii ya uongo akasema hayo yote anamuachia mungu coz gazeti ni la leo na litapita na litaenda watakua wamefurahisha nafsi zao tu lakini imemuuma sana kwa hili.

LAKINI pia alipoulizwa kuwa hii ni mara ya pili anaandikwa gazetini kuhusiana na hili huku ya kwanza ikiwa ni kuhusina na kukamatwa kwake kutokana na kifo cha Kanumba akasema yote wanaoyoandika hayana ukweli na kusema Lulu ni rafiki ake wa kawaida tu na wala hawana mazoea hayo.

MSIKILIZE CHALZ BABA HAPA
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII

Copyright © 2013. ArtAfropixels Media.com - All Rights Reserved
Customized by: IT XPERTTZ ONE | Powered by: BS
Designed by: Tilabs