AGNES MASOGANGE: "NINA UHURU WA KUTOA PENZI KWA MTU YEYOTE NINAYEMPENDA...."
MWANADADA anayejipatia umaarufu kupitia video za wasanii wa muziki wa kizazi kipya, Agness Masogange, alipoongea na mtandao wa MPEKUZI alifunguka na kusema kuwa hatumii mwili wake kama chombo cha kuwakamata wanaume bali hutoa penzi lake kwa yule anayempenda na ishu zinazozungumzwa mitaani kuwa anaongoza kwa kuiba wanaume za watu si kweli na wanaodai hivyo hawamtakii mema.
Alipoulizwa juu ya ishu kadhaa zinazongumzwa juu yake, ndipo alipofunguka kuwa hatumia uzuri wake au umbo lake kama njia ya kuwavuta wanaume kwani angeamua kufanya hivyo basi angekuwa na wanaume wengi sana.
“Mwili wangu si chombo cha kuwakamata wanaume na hao watu wanaosema kuwa naongoza kwa kutembea na wanaume za watu ni wale wenye nia ya kunichafua kwani mi si demu wa hivyo,” alidai
0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII