JACK WOLPER ATWAA TAJI LA IJUMAA SEXIEST GIRL ............SOMA ZAIDI HAPA
Jacqueline
Wolper (kulia), akipokea cheti cha ushindi kutoka kwa DK. Cheni
aliyekuwa jaji mkuu wa shindano hilo. Wolper akiwa ameshikiria cheti
chake muda mfupi baada ya kutangazwa mshindi. Dok. Cheni akiwa kwenye pozi na Wolper juu ya jukwaa. Msanii wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz akiwajibika jukwaani na mnenguaji wake.
Dogo Asley akiwajibika.
MSANII
wa chimbo la filamu Bongo, Jacqueline Wolper Masawe, usiku wa kuamkia
leo ameibuka kidedea kwenye shindano lililokuwa likiwashirikisha mastaa
wa kike Bongo la Ijumaa Sexiest Girl ndani ya Ukumbi wa Dar Live Mbagala
jijini Dar es Salaam.
Wolper amejizolea heshima lukuki na kitita cha sh. milioni 2 ikiwemo na ofa ya kulipiwa saluni kujiremba kwa mwaka mzima. Usiku
wa leo pia ndani ya ukumbi huo kulikuwa na burudani kibao kutoka kwa
Ommy Dimpoz, Chidy Benz, Dogo Asley, TOT Taarab na michezo kibao ya
watoto iliyosindikizwa na shindano la Mkali wa Mic.
0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII