LUCY KOMBA APATA SHAVU LA KUFANYA FILAMU NCHINI DENMARK

STAA wa sinema za Bongo, Lucy Francis Komba amekula shavu la kufanya filamu nchini Denmark kwa miezi mitatu hadi mwakani.
Akichonga na Mtandao wa MPEKUZI hii juzikati, jijini Dar akiwa njiani kuelekea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar ambako aliondoka na Ndege ya Scandinavia Airways, Lucy alisema:
“Ni kweli nasafiri, nakwenda Denmark kucheza filamu. Nitakuwa kule kuanzia Oktoba hii, Novemba, Desemba na Januari.”
Miezi ya hivi karibuni, Lucy amekuwa akienda kufanya ‘shooting’ ya filamu nje ya nchi. Katikati ya mwaka huu, alikwenda Ghana, Nigeria na baadaye Burundi.
0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII