‘SINTAH’ AKANA UWEPO WA PICHA ZAKE ZA UTUPU, ASEMA MWENYE NAZO AZIWEKE HADHARANI…!!

Lipo kundi la watu kadhaa linalodai kuwa wana picha za msanii huyo zinazomuonesha mwili wake ukiwa mtupu kama alivyozaliwa huku ikidaiwa kuwa picha hizo alipigia nchini Marekani na baadhi yake zilitumika kwenye movie kadhaa za utupu.

J Lo wa bongo katika pozi
Alisema kuwa mara nyingi safari zake za nje huwa si kwa ajili ya kufanya upuuzi kama huo bali anaenda kwa ajili ya kazi hivyo baadhi ya watu wanaona wivu na ndiyo maana wanazusha habari ambazo hazileti picha nzuri kwani jamii.
“Mimi ni jeshi la mtu mmoja hivyo wanapoona mafanikio yangu yanakuja wanaanza kuleta habari zao za kumchafua mtu, nawaambia tu kwamba sitishiki na nitazidi kusonga mbele na hao wanaosema hivyo watabaki na umaskini wao,” alisema.
0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII