WATUHUMIWA WA MAUAJI YA KAMANDA BARLOW WATIWA MBARONI....SOMA ZAIDI HAPA
BONGONEWZ BLOG

Majina ya watu matano wanaotuhumiwa kuhusika moja kwa moja na kifo cha Polisi Mkoa wa Mwanza, Leberatus Barlow yametajwa rasmi leo jijini Mwanza.
Akitaja majina hayo mbele ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania IGP Said Mwema, MKURUGENZI wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), Robert Manumba, amesema kuwa simu iliyoporwa ya mwanamama ambaye alikuwa akisindikizwa nyumbani na marehemu ndiyo imesaidia kukamilisha upelelezi huo hatimaye wahusika kukamatwa...
DCI Manumba ameyatangaza majina ya wahusika hao kuwa ni Muganyizi Petro (36) ambaye inatajwa kuwa ndiye aliyemuua Barlow, Chacha Mwita (50), Magige Mwarwa, Edward Masota pamoja na Bhoke Mwita ambao wote wamekamatiwa jijini Dar es Saalm.
Alisema kikosi cha nguvu kazi kilichokua chini yake Manumba kilijigawa kwenye makundi matatu moja ni lile la Ukamataji, Mahojiano na lingine la interejensia huku wakitumia njia ya sanyansi kwa kufuatia mitandao ya simu.
Kukamatwa kwa watuhumiwa hao wa dar na wale wa Mwanza kunafanya jumla yao kuwa 10 na bado jeshi linasaka wengine. Lakini hakuna sababu iliyotokana na mauaji hayo ambayo imeelezwa mpaka sasa na jeshi hilo.
Liberatus Barlow aliuawa Oktoba 13 mwaka huu, saa 8 usiku kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana katika eneo la Minazi mitatu huko Kitangiri wakati alipopita kumsindikiza Mwalimu Dorothy Moses nyumbani kwake kutoka katika kikao cha harusi kilichofanyika Mtaawa Rufiji.

0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII