WAZIRI MULUGO AZUNGUMZA KUHUSU ALICHOKIFANYA HUKO S.A, SOMA ALICHOJITETEA HAPA
BONGONEWZ BLOG


Kuanzia juzi taarifa na video
ya Naibu Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi wa Tanzania Philipo
Augustino Mulugo zimeanza kusambaa kwa watanzania wengi kuhusu
alichosema akiwa Afrika Kusini kwenye mkutano wa kimataifa kwamba
Tanzania ni muungano wa visiwa vya bahari ya Hindi, Pemba na Zimbabwe.
Mulugo leo amezungumza na Power
Breakfast ya CLOUDS FM na kusema kabla ya yeye kupanda kuanza
kuzungumza kulikua na kiongozi wa Zimbabwe ambae alitoka kuzungumza na
nina mkariri akisema “sasa ilibidi lazima baada ya kufika pale ni lazima
umshukuru mwenzako aliepita sasa kama mawazo ndiyo yaliyokua
yamedhania hivyo kwamba basi hapa naitamka Zimbabwe kwa sababu zote
zimeanzia na ZZ labda ilitokea hivyo lakini nakiri kabisa kwamba sikua
na makusudio kwamba naitamka Zimbabwe lakini kule kwenye power
presentation inaonekana kabisa ukifungua pale ni Tanzania imeungana na
Zanzibar Pemba na Tanganyika kama ambavyo tunajua kwa sababu ile ni
histori hakuna asiejua hata mtoto wa darasa la tatu”
“Niseme tu kwamba hiyo ni
kuteleza kwa ukimwi na nilikua namfikiria yule waziri wa Zimbabwe kwa
sababu alikua ametoka kuhutubia kabla ya mimi, nilikua naomba ieleweke
hivyo………… na wengi wameongea wanahoji lugha kiingereza, jamani
tukubaliane kwamba kusema Zimbabwe badala ya Zanzibar sidhani kama
inaendana na drama yenyewe kwa sababu mimi nimekua mwalimu mda mrefu
nimefundisha wanafunzi wangu na wananifahamu uwezo wangu mkubwa na tena
mimi ni mwalimu wa historia hata degree yangu ni mimi ni mwalimu wa
historia na economics, labda niliongea nilikua sijielewi na ningegundua
nimetamka Zimbabwe ningeweza kuomba radhi, mataifa
yote wawe waafrika wawe wazungu wengi huwa tunazingatia kuangalia
kwenye power point pale, wengi huwa hawasikilizi sauti” – Mulugo
Kuhusu kukosea kutaja mwaka,
Namkariri naibu waziri akisema “mimi pale nia yangu ilikua ni kusoma
namba moja moja nikashtukia nakwenda kusoma mbili haijakaa kama
nimekosea kiingereza kama watu wanavyoipanua kwa mfumo huo lakini kama
watu wamenielewa hivyo niombe tu msamaha”

0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII