BREAKING NEWS: SHARO MILIONEA AFARIKI DUNIA KWA AJALI YA GARI, KAMANDA WA POLISI ATHIBITISHA
MSANII WA VICHEKESHO NA MUZKI SHARO MILIONEA AMEFARIKI LEO HUKO MUHEZA TANGA KWA AJALI YA GARI AMBAPO NDUGU YAKE WA KARIBU SNURA MUSHI AMETHIBITISHA TUKIO HILO KWA NJIA YA SIMU .....
Naye Kamanda wa Polisi mkoani Tanga, Afande Constatine Masawe, amethibitisha kutokea kwa kifo cha wa Sharobaro, kufuatia ajali ya gari katika kijiji cha Lusanga, Muheza, mkoani Tanga ambako ndio nyumbani kwao.......
MPAKA SASA MWILI UPO HOSPITALI TEULE YA MUHEZA ,TANGA
Akizungumza na simu na Millard Ayo wa Clouds FM RPC wa mkoa wa Tanga alisema: "“leo majira ya saa mbili usiku kwenye barabara ya Segera Muheza mtu mmoja alietambulika kwa jina la Hussein Ramadhani Mkiety au Sharo Milionea akiwa anaendesha gari namba T478 BVR Toyota Harrier akitokea Dar es salaam kwenda Muheza alipofika eneo hilo gari lake liliacha njia na kupinduka mara kadhaa na kusababisha kifo chake, mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali Teule ya wilaya ya Muheza.”
Kwa taarifa zaidi endelea kutembea mtandao huu kujua taratibu za mazishi za msiba huu mkubwa kwenye tasnia ya burudani nchini Tanzania
0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII