FAINALI ZA EBSS NA BEI YA VIINGILIO VYAKE....INGIA HAPA USOME


 Ijumaa hii Tanzania itashuhudia washiriki wa 5 waliobaki katika shindano kubwa la kutafuta vipaji vya kuimba hapa nchini EBSS wakipanda kwenye stage ya Daimond Jubilee ambako mshindi ataondoka na pesa taslimu shilingi milioni 50.Usiku huo wa fainali za shindalo hilo la EBSS  ambalo mwaka huu limedhaminiwa na Kampuni ya simu ya Zantel  na lilikuwa likitumia kauli mbiu ya 'FUNGUKA' utapambwa na na burudani kutoka kwa wasanii wakubwa hapa Tanzania kama Mwasiti,Rich Mavoko,Amini,Linah,Ben Pol,Barnaba,Banana Zorro,Linex, Mzee Yusuph,Haji Ramadhani, Laila Rashid na Ditto.
Barnaba mmoja ya wasanii watakaoperfom siku hiyo
Viingilio kwenye fainali za EBSS ni bei ya rahisi sana ambayo naamini kila mtanzania akijipanga ataweza kuja kushuhudia huyo mshindi atakayeondoka na Milioni 50 na burudani zingine kibao.VVIP ni pesa za Kitanzania shilingi elfu 70,VIP Elfu 30,na viti vya kawaida ni shilingi Elfu 10 tuu. Kwa booking unaweza ukapiga namba hii hapa+255 778 952 795.
 Moja ya majaji wa shindano hilo la EBSS Salama J
Ticket za fainali za EBSS zinazofanyika dis Friday pande za Daimond Jubilee kuanzia mida ya 1 nakuendelea, zinapatikana katika  maeneo yafuatayo
     SHEAR ILLUSIONS – MILIMANI CITY .
    BIGGY RESPECT- KARIAKOO.
     STEERS- MJINI (CITY CENTRE).
   ZIZZOU FASHION (VICTORIA & SINZA).
  PHOTOPOINT- MAYFAIR PLAZA.
     ROBY ONE FASHIONS (KINONDONI).
  BEST BITE.
   SAMAKI SAMAKI- MBEZI.
   DIAMOND JUBILEE HALL.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII

Copyright © 2013. ArtAfropixels Media.com - All Rights Reserved
Customized by: IT XPERTTZ ONE | Powered by: BS
Designed by: Tilabs