Homa ya uchaguzi wa Marekani yazidi kupanda wakati kampeni zikifikia ukingoni
Kampeni
za lala salama nchini Marekani zimeendelea huku Rais Barack Obama na
hasimu wake kisiasa Mitt Romney wakiendelea kujinadi kwa wananchi lengo
likiwa ni kusaka kura ambazo zitawapeleka katika Ikulu ya White House.
Baada ya kampeni za miaka miwili nchini Marekani wananchi wa
Taifa hilo wanatarajiwa kupigakura kesho tarehe sita kuamua nani atakuwa
Raisi.
Kwa upande wake Romney ambaye ni kinara wa kukosoa sera za Rais Obama
hakurudi nyuma kwenye harakati zake na badala yake akabainisha kwa
wananchi kile ambacho kimeshindikana kwenye utawala wa Obama hususan
akizungumzia changamoto ya ajira.
Wachambuzi wa Siasa wanaendelea kumpa nafasi Rais Obama kuweza kutetea
wadhifa wake huku suala la kushughulikiwa kwa madhara ya kimbunga cha
sandy likionekana kumuongezea sifa raisi Obama.
Wananchi wa Marekani wameshaanza kupiga kura mapema wengi wao wakiwa ni
wanachama wa Chama Cha Democratic huku kura za Jopo zinazopigwa kutoka
kila Jimbo ndizo ambazo zitaamua nani awe Rais.
0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII