Lowassa azungumzia Rushwa katika Chaguzi za CCM...SOMA HAPA
Kwa wale mliotaka kujua kama Lowassa akiwa Rais atakuja kukemea rushwa,
Mzee huyu amewasikieni, hapa ni maelezo yake kuhusu Rushwa kwenye
chaguzi za CCM kama alivyonukuliwa leo Jumanne na Gazeti la Mwananchi.
Lowassa azungumzia rushwa.........
Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa ambaye kwa sasa yuko Ujerumani kuchunguzwa afya yake, ameeleza kusononeshwa kwake na habari za rushwa zilizokithiri ndani ya CCM.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Lowassa alisema: “Nikiwa mwanaCCM na Mtanzania, ninasononeshwa sana na taarifa za kukithiri kwa vitendo vya rushwa ndani ya chama chetu, serikalini na katika taasisi mbalimbali.
“Ni kweli kwamba, rushwa ni tatizo. Ni kansa ambayo kama taifa, hatuna budi kulitafutia ufumbuzi wa kimfumo badala ya kuendelea kufikiri kwamba linaweza kumalizwa kwa njia ya kulalamika, kulaumiana na kupakana matope.
“Tunao wajibu wa kuhakikisha kwamba Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), inapewa meno na kuimarishwa zaidi katika kukabiliana na vitendo hivi vya ukiukwaji wa maadili.”
Akizungumzia afya yake Lowassa alisema: “Ninamshukuru Mungu siha yangu ni imara na kwamba madaktari walionifanyia uchunguzi wamejiridhisha pasi na shaka kwamba afya yangu ni njema.
“Ninaendelea na matibabu mazuri katika jicho langu moja ambalo nilifanyiwa upasuaji miaka miwili iliyopita hapahapa, (Ujerumani), ninatarajia kurejea nyumbani wakati wowote kuanzia sasa kuungana na Watanzania wenzangu katika kulijenga taifa letu.”

0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII