HUYU NDIO MSHINDI WA EBSS MWAKA 2012.......PATA HABARI KAMILI KUHUSU YALIYOJILI

Photo: #EBSSFinale - mambo motoooo!
 


Zile fainali zilizokuwa zinasubiliwa kwa hamu sana na watanzania kwa ajili ya kumjua mshindi wa Epiq Bongo Star Search (EBSS) zi memalizika usiku huu, mshiriki Walter Chilambo ndio ameibuka kidedea katika kinyang'anyiro hicho kwa kuwabwaga wenzie watano ambao walikuwa wamebaki katika fainali hiyo. Photo: LIKE kuwapa presenters wetu Caesar Daniel na Vanessa Mdee big up! #EBSSFinale

Japokuwa Walter ameibuka mshindi lakini alikumbana na ushindani mkali sana kutoka kwa washiriki wenzie wawili ambao wote walifanikiwa kuingia 3 bora ambao ni Wababa kutoka Dar es salaam pamoja na Salma kutoka Zanzibar. Kutokana na ushindi huo, Walter amejinyakulia pesa taslimu shilingi milioni hamsini (mil 50) kutoka kwa wadhamini wa mashindano hayo kampuni ya simu za mkononi ya Zantel. Mashindano hayo ambayo hufanyika kila mwaka yameonekana kufana zaidi kushinda mashindano yaliyotangulia. Photo: Unadhani nini kilikuwa kinaendelea hapa....? #EBSSFinale

Akihitimisha shindano hilo mkurugenzi wa kampuni ya BENCHMARK PRODUCTION ambao ndio waandaaji wa mashindano hayo kila mwaka, Madam Rita Paulsen aliwashukuru wote waliofanikisha shughuli hiyo huku shukrani nyingi zikienda kwa wadhamini wao ambao wameonyesha utofauti mkubwa katika shindano la mwaka huu...

HONGERA SANA WALTER CHILAMBO HAKIKA KIPAJI CHAKO KIMEONEKANA
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII

Copyright © 2013. ArtAfropixels Media.com - All Rights Reserved
Customized by: IT XPERTTZ ONE | Powered by: BS
Designed by: Tilabs