MAMA YAKE RAY C AFUNGUKA NA KUSEMA RAY C ANAHITAJI KUSAIDIWA...!!!
Mwanamuziki
wa kike Rehema Chalamila maarufu kama Ray C kwasasa anaishi maisha
magumu baada ya kuathiriwa na kinachosemekana kuwa ni matumizi ya
madawa ya kulevya kwa muda mrefu.
Mwanadada
huyo maarufu kama kiuno bila mfupa hivi karibuni alihamishia makazi
yake mjini Nairobi, Kenya, na aliporejea nchini hali yake ilikuwa mbaya.
Mama
mzazi wa Ray C, Bi Margret Mtweve alifunguka kwa njia ya simu na
kuzungumza na Mo Bloga na kusema amesikitishwa na kitendo cha vyombo vya
habari kuandika tu hali ya Ray C bila kuhamasisha msaada..
“Kwa
kweli mwanagu ninae nyumbani kwasasa nalala nae kabisa, na nimeokoka
namuombea sana kwa Mungu, na ninaamini Mungu ni mwema atamsaidia”
alisema Bi Margret nakuongezea.
“Mwanangu
aliwasaidia watu wengi lakini sasa hivi anamatatizo sioni mtu hata
mmoja wakuja kunipa msaada, zaidi ni simu za waandishi kutaka habari za
kumchafua”
Mama Ray C yuko tayari kupokea msaada wowote kutoka kwa wanajamii na namba yake ya simu ni 0655 999 700 waweza mtumia hata kwa Tigo Pesa.
0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII