TANZANIA MITINDO HOUSE YAADHIMISHA MIAKA MITANO KWA CHAKULA CHA MCHANA PAMOJA NA WATOTO YATIMA.
"Nyota Njema huonekana Alfajiri". Watoto wanaoelekea kuwa Wanamitindo wa baadae wakiweka pozi mbele ya Camera yetu.
Tanzania
Mitindo House imefanya sherehe ya kusheherekea miaka mitano tangu
kuanzishwa kwa kula chakula cha mchana na watoto yatima kutoka ‘Malaika
Orphanage Center’ na ‘Umraa Orphanage Center’ katika kituo chao cha
kuchezea watoto yatima kilichopomanispaa ya Temeke.Pichani Juu na Chini
ni Watoto wakicheza michezo mbalimbali katika sehemu maalum ya Tanzania
MitindoHouse Fun Centre. Sherehe hizo zimedhaminiwa nan KIONDO
COMMUNICATIONS INTERNATIONAL, AMAYA BEAUTY SALOON NA AIM GROUP.
Pichani
Juu na Chini ni Watoto wa Kituo cha kulelea watoto yatima cha Tanzania
Mitindo House (wenye sare za mashati ya Vitenge vinavyotengenezwa na
kiwanda cha Morogoro Polytex kilicho chini ya Makampuni ya MeTL)
wakisakata Kabumbu walipojumuika na watoto wenzao wa vituo vingine
katika kusheherekea miaka 5 ya kituo chao.
Pichani
Juu na Chini watoto wa kike nao walipata fursa ya kuchangamsha viungo
kwa kucheza Netball katika kituo cha Mitindo House Fun Centre Kigamboni
Jijini Dar es Salaam.
Jumping Castles lilikuwepo pia.
Mwenyekiti
wa Kituo cha Tanzania Mitindo House (TMH) Bi. Khadija Mwanamboka
akikata keki pamoja na Watoto wa kituo chake cha kulelea watoto yatima
katika kusheherekea miaka 5 tangu kuanzishwa kwa kituo hicho ambacho
mpaka sasa kina jumla ya watoto 10 saba wakiume na watatu wakike.
Mtoto
Ashraf Kombo Mwanafunzi wa shule ya msingi ya Almuntazir alitumia fursa
hiyo kusheherekea siku yake ya kuzaliwa na watoto yatima wa kituo cha
Tanzania Mitindo House (TMH) kilichotimiza miaka 5 mwishoni mwa wiki.
Mama mzazi wa Ashraf akilimlisha keki mwanae mpendwa.
Mtoto Ashraf akimlisha keki mmoja wa watoto waliohudhuria sherehe hiyo.
Kwaito ilichezeka.
Na Kiduku pia.
Pichani
juu na Chini ni Muda wa Msosi ulifika ni kitu cha Biriani tena....
Watoto wa ‘Malaika Orphanage Center’ , ‘Umraa Orphanage Center’
'Tanzania Mitindo House' na walezi wao.
Mwenyekiti wa TMH Bi. Khadija Mwanamboka katika Picha ya pamoja na ugeni wake.
0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII