TEMBA NAYE AIBIWA VIFAA VYA GARI LAKE, WEZI WADAI WATAENDELEA KWA KUIBA KWA WASANII NA WATANGAZAJI
Alfajiri ya kuamkia leo, Mh Temba ameibiwa vifaa vya gari lake aina ya
verossa akiwa amelipaki nyumbani kwake Temeke.Temba amesema
vifaa vilivyoibiwa ni pamoja na power window, side mirror zote taa za
nyuma, radio leseni,na vinginevyo ambavyo thamani yake hajaijua kwa
sasa.
"jamaa siwajui ila wamekuja na wameniibia power window, taa za nyuma, sidemirror vitu vya ndani wameiba radio, leseni hadi madaftari yangu ya shule, makaratasi, sasa sijui atakua ametumwa au anafanya maksudi yaani anaiba mpaka madaftari" amesema temba
lakini baada ya wizi huo temba alipiga simu polisi na kati ya info alizopewa na washkaji zake walio central si unajua jamaa likua mwanajeshi kitambo sasa baada ya kuongea na watu wa usalama alipewa ripoti kuwa kuna watu wameamua kuwakomoa wasanii pamoja na watangazaji, kwa kuwaibia mpaka mwenzao alieshikiliwa aachiwe
" kituoni sasa hivi mishe mishe zilizokuwepo ni kwamba kuna jamaa wametangaza kwamba wanaibia wasanii wote magari na mapresenter nao watakoma mpaka mtu wao wakaribu aachiwe, naskia kuna mtu wao ambae wanafanya nae kazi amekamatwa yuko ndani wamesema kwamba wataibiwa wasanii wote na vitu vya magari kwasababu ndio wamesababisha mtu wao amewekwa ndani..." amesema temba
weekend iliyipiya msanii Suma lee aliibiwa gari lake aina ya Land cruser VX yenye thamani ya shilingi milioni 70 maeneo ya coco beach alipokuwa amelipaki na mpaka leo hii halijapatikana tukio lililotokea wiki kadhaa baada ya gari la Ommy Dimpoz kuibiwa vifaa pia
Temba alimalizia kwa kusema, kama angepata nafasi ya kuwakamata wezi hao basi angewatembezea kvipara raaaaaah
0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII