RAIS JAKAYA KIKWETE AZINDUA TAASISI SAYANSI NA TEKNOLOJIA YA CHUO KIKUU CHA NELSON MANDERA ARUSHA
Rais
Jakaya Kikwete, akikata utepe kuweka jiwe la Msingi ikiwa ni ishara ya
kuzindua rasmi Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Chuo cha Kikuu cha
Nelson Mandera, jijini Arusha leo, Novemba 02, 2012. Kushoto kwake ni
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mkuu wa Chuo hicho,
Dkt. DMohammed Gharib Bilal. Kushoto ni Makamu wa Mkuu wa Chuo hicho,
Profesa Burton Mwamila.
Rais Jakaya Kikwete, akifunua kitambaa ikiwa ni ishara ya kuzindua
rasmi Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Chuo cha Kikuu cha Nelson
Mandera, jijini Arusha leo, Novemba 02, 2012. Kulia kwake ni Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mkuu wa
Chuo hicho, Dkt. DMohammed Gharib Bilal. Kulia ni Makamu wa Mkuu wa Chuo
hicho, Profesa Burton Mwamila.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mkuu wa Chuo cha Nelson Mandera, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda mti wa kumbukumbu wakati wa hafla ya uzinduzi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Chuo cha Kikuu cha Nelson Mandera, jijini Arusha leo, Novemba 02, 2012. Kulia ni Rais Jakaya Kikwete, aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo.
Rais Jakaya Kikwete, akimkabidhi Makamu wake na Mkuu wa Chuo cha Nelson Mandera, hatimiliki ya Ardhi ya chuo hicho wakati wa hafla ya uzinduzi wa chuo hicho iliyofanyika leo Novemba 02, 2012 jijini Arusha. Kuliani ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Burton Mwamila.
Rais Jakaya Kikwete, akipokea zawadi ya picha kutoka kwa Makamu wake na Mkuu wa Chuo cha Nelson Mandera, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Burton Mwamila, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Taasisi ya Sayansi
na Teknolojia ya Chuo cha Kikuu cha Nelson Mandera, jijini Arusha leo,
Novemba 02, 2012. Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII