TUME YA NGWILIZI YAWASAFISHA WABUNGE WALIOTUHUMIWA KUJIHUSISHA NA RUSHWA
Maswi aliwatuhumu moja kwa moja baadhi ya wabunge kwa
maandishi kutaka rushwa na wakimtishia kupoteza nafasi yake ya Ukatibu
wa Wizara
Tume inasema Maswi alitoa tuhuma hizi kwa lengo la kujihami juu ya tuhuma zilizokuwa zinamkabili
Tuhuma za kuwa Maswi aliombwa rushwa ya Milioni 50 na wabunge nazo zimetupiliwa mbali kuwa lengo ni kutaka kujihami.
Mbunge Selasini alipohojiwa na Tume, alikiri kuwa hakuwa na ushahidi wa maneno 'aliyoropoka' bungeni akiwatuhumu baadhi ya wabunge waliohisiwa kupokea rushwa.
Mnyika alipohojiwa juu ya kauli yake Bungeni kuwa Maswi anashinikizwa ajiuzulu nafasi yake, Mnyika alitumia ushahidi wa vyombo mbalimbali vya habari! Anadai kuwa hakukuwa na kanusho la habari hizo (labda ndilo lilimpelekea kuamini ni habari sahihi)
Ole Sendeka alipohojiwa juu ya kauli yake bungeni; alidai kuwa alikuwa anajaribu ku pre-empty tu.
Mbunge Kessy naye alijikanyaga tu kuwa lazima kulikuwa na rushwa tu
Waziri Muhongo alipohojiwa na Tume alisema ni 'allegations' tu.
Mbunge Sarah Msafiri na mwenzake wamesafishwa, hawakuiuzia TANESCO matairi! Tuhuma za Tundu Lissu pia zimeonekana kukosa mashiko na amekiri kuwa alipata taarifa toka kwa watu wa Wizara, hakuwa na ushahidi wa moja kwa moja!
Wabunge waliotoa tuhuma bungeni, wamekemewa na kutakiwa kutorudia tena.
Lissu amekaripiwa vikali kwa kuwachafua wabunge na waliochafuliwa wameombwa wamsamehe bure.

Waziri Sospeter Muhongo amekaripiwa kwa kuwachafua wabunge na ametakiwa awe mwangalifu anapotoa kauli yoyote bungeni kwakuwa kauli yake inachukuliwa ni kauli ya Serikali.
0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII