MBOWE ATOA TAMKO, ASEMA ATAISIMAMISHA NCHI TAREHE 25 KWA MAANDAMANO YA NCHI NZIMA....SOMA SABABU NI NINI
Muda mfupi uliopita hapa katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mkendo,
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe, ametoa tamko la Musoma,
likiwataka Watanzania wote wapenda nchi yao, kujiandaa kwa maandamano
makubwa na mgomo wa wananchi yatakayofanyika Machi 25, 2013, nchi nzima,
kushinikiza uwajibikaji (kujiuzulu au kufukuzwa kazi) kwa Waziri wa
Elimu na Mafunzo ya Ufundi Shukuru Kawambwa na Naibu wake, Phillip
Mulugo, kutokana na matokeo mabaya ya kidato cha nne.
"Yatakuwa maandamano makubwa ya kuisimamisha nchi...tunataka siku hiyo
mama ntilie wawe barabarani, watoto waliofeli na wazazi wao wawe
barabarani, bodaboda wawe barabarani, wamachinga wawe barabarani, walimu
wawe barabarani, wanafunzi walioko shuleni na vyuoni wawe barabarani,
askari watuunge mkono.
"Wazalendo wote watuunge mkono, Machi 25, 2013, Watanzania wawaoneshe
watawala kuwa sauti ya wananchi ni kubwa na muhimu kuliko waziri mmoja
na naibu wake...tunataka kitu kidogo tu, waziri na naibu wake wajiuzulu,
tunataka wawajibike kwa matokeo mabaya ambayo yametuingiza kwenye
kitabu cha maajabu ya dunia..., wanaume na wanawake siku hiyo hakuna mtu
kubaki ndani.
"Tutaisimamisha nchi katika majiji manne, Dar
es Salaam, Mbeya, Mwanza na Arusha...nanyi wa Musoma mnataka kulianzisha
hapa? Haya Mbunge Nyerere wananchi wako nao wamesema watalianzisha hapa
hapa, hawataki kuja Mwanza, kwa hiyo wa Butiama watashuka Musoma, wa
Tarime watashuka hapa, wa Serengeti, Bunda na Mwibara, watashuka hapa,
yataanzia wapi na kuelekea wapi, mtaambiwa hatua za baadae. Wananchi
mjiandae Machi 25, maandamano na mgomo mkubwa," alisema Mbowe.
More updates to come...
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII