HII NDIO MOVIE YA KANUMBA ILIYOTABIRI KIFO CHAKE, ITAINGIA SOKONI KESHO. TAZAMA TRAILER YAKE HAPA

 
859448_441752602570850_900249450_o
Ile filamu ya Love & Power ambayo imekuwa ikisubiriwa kwa hamu na wapenzi wengi wa filamu hatimaye mwisho wa wiki hii siku ya Ijumaa tarehe 12th April 2013 itazinduliwa na kuingia sokoni rasmi na kusambazwa nchi nzima na kampuni ya mahiri ya usambazaji wa filamu ya Steps Entertainment Ltd.
Akizingumza na waandishi wa wanahabari mratibu wa filamu ya Love & Power Bwana Myovela Mfwaisa amesema kuwa  “Filamu ya Love & Power  ni filamu ya mwisho kutengenezwa na marehemu The Great Kanumba  inaingia sokoni na kuwafikia watanzania wote siku ya ijumaa,”
Hivyo basi hii itakuwa fursa pekee kwa wa tasnia ya filamu na watanzania wote kwa ujumla na kuweza kujionea kazi bora iliyotengenezwa na gwiji la filamu na balozi aliyetangaza tasnia ya filamu ya Tanzania nje ya mipaka ya Tanzania, kila mpenzi wa filamu aweke ahadi kutokuikosa filamu bora na ya mwisho kuigizwa na marehemu nyota wa filamu Tanzania.
Akizungumzia kwa ufupi juu ya filamu ya Love & Power Bwana Myovela, “Filamu ya Love & Power imetengenezwa na kampuni ya Kanumba the Great film kwa kushirikia na Steps Entertainment Ltd ikiwa imeandikwa na Ally Yakuti, Filamu ya Love & Power imeshirikisha wasanii nyota katika tasnia ya Filamu Tanzania kama Hussein Mkiety ‘Sharomilionea’, Irene Paul, Patcho Mwamba, Grace Mapunda, Hartman, Rammy Galis pamoja Seth Bosco ambaye ni mdogo wake na marehemu  kuongozwa na Steven Kanumba, Watayarishaji wakuu ni Steps Entertainment Ltd imetengenezwa hapa jijini Dar es Salaam katika maeneo  tofauti tofauti.
Lugha iliyotumika katika filamu hiyo ni Kiswahili lakini pia Lugha ya kiingereza imetumika  kama ‘Subtitles’. Umri wa kutazama filamu ya Love & Power ni miaka 16 ni filamu nzuri inayotazamwa na watoto pamoja na familia, iliyopewa kibali cha ukaguzi  Kutoka Bodi ya ukaguzi wa filamu na michezo ya kuigiza Tanzania.
Pichani kati ni mratibu wa filamu ya Love & Power Bwana Myovela Mfwaisa akizungumza na Wanahabari Mapema leo jijini dar.
Pichani kati ni mratibu wa filamu ya Love & Power Bwana Myovela Mfwaisa akizungumza na Wanahabari Mapema leo jijini dar.
Katika kuhakikisha kuwa wasanii wanafaidika na kazi zao tunaomba kila mdau wa filamu awe mlinzi wa kazi hizi za filamu za kitanzania kwa kupambana na Maharamia wa kazi za Wasanii wa filamu, pia tunawaomba wapenzi wa filamu kununua nakala halali yenye nembo ya Steps Entertainment Ltd, hiyo itachochea maslahi kwa wasanii wa Tanzania na kuongeza ajira kwa vijana ili kufikia hilo nunua filamu ya Love & Power halali.
Unaweza kupata filamu ya Love & Power kwa kuwasiliana na Wasambazaji kwa namba hizi:  0716 788 805, 0713 570 581
Asanteni.

TAZAMA TRAILER YAKE HAPA, NI NZURI SANA .....DONT MISS IT

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII

Copyright © 2013. ArtAfropixels Media.com - All Rights Reserved
Customized by: IT XPERTTZ ONE | Powered by: BS
Designed by: Tilabs