TAZAMA PICHA ZA TUKIO LA VURUGU ZILIZOTOKEA TUNDUMA, HAKIKA TANZANIA IMECHAFUKA SASA
Hii ndiyo hali halisi ya Mji mdogo wa Tunduma leo kuanzia asubuhi
Matairi yanachomwa katikati ya barabara

Mambo hayo 
Mwandishi
  wetu pamoja na waandishi wenzake walipata shida sana kufika  
mji wa Tunduma walikutana na vikwazo vingi sana lakini wananchi walikuwa
  waelewa waliwasaidia kutoa magogo na matairi ili wapite wakapate 
habari
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Diwani akiongea na waandishi wa habari
Wanafunzi wakisindikizwa na jeshi la polisi kurudi majumbani mwao
Polisi wakiendelea na kazi yao katika mitaa ya Tunduma
Baadhi ya magari ya IT yaendayo nchini Zambia yakiwa yamepakiwa nnje kidogo ya mji wa Tunduma kuogopa kuharibiwa kwa magari hayo
----------------
Diwani
 wa kata ya Tunduma Ndugu Frank Mwaijoka (Chadema) pamoja na mchungaji 
wa kanisa la KKT katika eneo hilo la Tunduma wilayani momba Mkoani mbeya
 wametakiwa kujisalimisha kituo cha Polisi Tunduma mara baada ya 
kuhusika na uchochezi wa kidini hali ambayo imepelekea kutokea kwa 
vurugu  katika eneo hilo.
Vurugu
 hizo zimeanza majira ya saa 4 asubuhi katika eneo hilo la tunduma mara 
baada ya kundi la watu wanaodai kuwa wao ni wafuasi wa dini ya kikristo 
wakidai waruhusiwe kuchinja mifugo na kuuza katika mabucha yao hali 
iliyo pelekea kuibuka kwa vurugu hizo.
Akizungumza
 kuhusiana na tukio hilko Kamanda wa Polisi Mkoani humo Ndugu Diwani 
Athumani amesema kuwa kufuatia kuwepo kwa tukio hilo jumla ya watu zaidi
 ya 40 tayari wamekwisha kamatwa .
Amesema
 mpaka sasa taarifa walizo zipata kufuatia vurugu hizo zinaeleza kuwa 
miongoni mwa watu walichochea vurugu hizo ni diwani wa kata hiyo ya 
Tunduma Ndugu John Mwaijoka pamoja na Mchungaji wa kanisa la kkt ndugu 
Neema Mwaipusa ambao kwa pamoja wametakiwa kujisalimisha kituo cha 
polisi kwa mahojiano zaidi.
Amesema
 suala hilo limegubikwa  na siasa kwani tayari viongozi wa serikali 
akiwemo Mkuu wa mkoa huo Ndugu Abbas Kandoro amekwisha litolea ufafanuzi
 Apri 02 mwaka huu wakiwepo pia viongozi wa dini .
Amesema
 kwa asilimia kubwa mgogoro huo juu ya nani achinje umeingiliwa na mambo
 ya kisiasa kwani hata baadhi ya wananchi wa maeneo hayo wamekuwa 
wakilalamika juu ya kutokea kwa vurugu hizo.
Amesema
 shughuli za kibiashara katika eneo hilo zimeshindwa kufanyika katika 
eneo hilo hivyo kufanya wananchi kupata adha hasa kwa nchi jirani ya 
Zambia ambao kwa asilimia kubwa wanategema kupata mahitaji kutoka 
mpakani mwa Tanzania.
Hata hivyo Diwani amesema kuwa katika 
vurugu hizo askari mmoja  pamoja na mwananchi wamejeruhiwa kwa kupigwa 
mawe ambapo tayari wamekwisha fikishwa kituo cha polisi.
Kufuatia
 hali hiyo Kamanda huyo wa Polisi amesema kwa sasa hali imelejea katika 
hali yake ya kawaida hivyo amewataka wananchi wa maeneo hayo kuwa 
watulivu wakati jeshi hilo la Polisi likiendela na msako wa kuwatafuta 
wahalifu wengine.


kila mtu achinje kwa imani yake na mabucha yaandikwe. kama ni ya waislamu yajulikane na ya wakristo pia. si vizuri kuongozwa na imani ya mtu mwingine
ReplyDelete