WEMA AZUA GUMZO HUKO ARUSHA....APEWA ULINZI MKALI, SOMA STORY KAMILI HAPA
Stori:Imelda Mtema
Kwa mara nyingine staa mkubwa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu anatengeneza kichwa cha habari baada ya kuacha historia jijini Arusha kufuatia ulinzi mkali aliokuwa nao, Ijumaa lina data zote.

Ilifahamika kuwa ndani ya ndege hiyo ambayo kuikodisha ni mkwanja mrefu, aliongozana na kampani yake tu.

Ilibumburuka kuwa timu yake hiyo ilikuwa takriban watu watano ambao walimsindikiza kwenda kwenye mapumziko kutokana na ‘stresi’ alizokuwa nazo.

Baada ya kutokea kwa ishu hiyo ndipo Wema alipoamua kwenda kujichimbia Arusha kupoteza mawazo.


Walipoingia jijini Arusha, staa huyo wa Filamu ya The Super Star alipokelewa kwa ulinzi mkali hadi katika hoteli ya bei mbaya aliyokuwa ameweka oda kwa ajili yake na watu wake.
“Unaambiwa kuanzia Arusha Airport (uwanja wa ndege) hadi hotelini ilikuwa ni full ulinzi wa kufa mtu,” kilisema chanzo chetu,
APOKEA MWALIKO
Habari zilieleza kuwa akiwa hotelini hapo, habari zilienea kama moto wa kifuu kuwa yupo jijini Arusha hivyo akapokea mwaliko kutoka kwa mashabiki wake waliotaka japo kumuona tu kwenye Fashion Show iliyoandaliwa.
KASHESHE
‘Eventi’ ilifanyika kwenye Ukumbi wa Club D (World Garden) uliopo jijini humo na ndipo kasheshe lilipoibuka kwa watu kukanyagana wakitaka kumuona na kupiga naye picha.
“Aisee Wema wee acha tu! Kusema kweli watu wanampenda sana. Kuna wakati niliona kama ukumbi unakuwa mdogo na kwa taarifa yako ilikuwa haijatangazwa. Sijui kama ingekuwa imetangazwa kuwa Wema yupo A-town, ingekuwaje maana kila mtu alitaka japo amshike tu,” alisema sosi wetu huyo.
MENEJA
Kwa mujibu wa meneja wake, Martin Kadinda, ilibidi kuomba ulinzi maalum wa mabaunsa ambao walihakikisha hadhuriki.
“Tuliwaambia tupo na mtu mkubwa sana hivyo tukapatiwa ulinzi maalum wa kuhakikisha Wema hapati tatizo la mtu kumdhuru na ndicho tulichokifanya,” alisema Kadinda.
Ilifahamika kuwa kwa harakaharaka ulinzi wa Wema ulikuwa na takriban watu wasiopungua 10, yote ikiwa ni kuhakikisha usalama wake.
AFANANISHWA NA KIM KARDASHIAN
Kwa mujibu wa mashabiki wake ukumbini hapo, ulinzi wa Wema ulifananishwa na ule wa staa wa Marekani, Kim Kardashian ambaye hivi karibuni aliwekwa mtu kati na watu zaidi ya 32 wakiwemo askari na mabaunsa.
“Kweli Wema sasa amefikia levo za akina Kim, yaani naye ana ulinzi mkubwa hivi?” alihoji mmoja wa mashabiki wake.
TIMU NZIMA
Ukimwacha Wema na Kadinda, wengine walioambatana nao ni Kajala Masanja, Petit Man ‘Wakuache’, Tinny Daddy na Nurdin Bilal ‘Shetta’.
Baada ya mapumziko wote walirejea jijini Dar na kuendeleza libeneke wakiwa ‘wamerefreshi’ akili.
NI KUFURU NYINGINE
Hii ni kufuru nyingine ya Wema ambapo swali liliendelea kubaki palepale kuwa anapata wapi fedha anazotumia katika matukio yake ya gharama kubwa huku nyuma yake kukiwa na madai kuwa kuna ‘mkubwa’ mmoja anamuwezesha.
Chanzo:www.globalpublishers.info
0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII