HABARI ZA KUSIKITISHA : MFANYABIASHARA AJIRUSHA KUTOKA GHOROFANI KARIAKOO NA KUFA HAPO HAPO...TAZAMA PICHA
Muda
 mfupi uliopita,Mtu mmoja alietambulika kwa jina la Shirima ambaye ni 
Mfanyabiashara katika moja ya Maduka ya Kariakoo jijini Dar es 
Salaam,amejirusha toka ghorofa ya 9 ya Hoteli ya Concord iliopo Maeneo 
ya Kariakoo jijini Dar es Salaam na amekimbizwa hospitali kwa uangalizi 
zaidi maana haijafahamika kama kapoteza Maisha au bado yu hai.
Mfanyabiashara
 huyo alijirusha toka ghorofani na kuangukia Gari aina ya Toyota 
Corolla ambayo ni taxi iliyokuwa imepaki nje ya hoteli hiyo....chanzo cha 
kujirusha kwa mfanyabiashara huyo bado hakijafahamika mpaka sasa.
Mashuhuda
 wa tukio hilo lililotokea muda mfupi uliopita,wanaeleza kuwa walipatwa 
na mshuko baada ya kusikika kishindo cha kitu kilichokuwa kimeangukia 
gari hilo na waliposogea kushuhudia ndipo walipobaini kuwa alikuwa ni 
mtu huyo alietambulika kwa jina moja la Shirima.
 
 

 
 

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII