HATIMAYE MASOGANGE NA MELISA WAACHIWA HURU.....SOMA ZAIDI HAPA
Johannesburg. Mtanzania Agnes Gerald, maarufu Masogange, ameachiwa huru na Mahakama ya Kempton ya jijini Johannesburg, baada ya kulipa faini ya R30,000 (Sh4.8 milioni) kwa kosa la kubeba kemikali zinazotumika kutengeneza dawa za kulevya.
Wakati Masogange akitozwa faini hiyo mwenzake,
Melissa Edward ameachiwa huru na mahakama hiyo, baada ya kukosekana
ushahidi wa kumtia hatiani.
Msemaji wa Kitengo cha Uchunguzi wa Makosa ya
Jinai cha Afrika Kusini(Hawk), Kapteni Paul Ramaloko alisema Watanzania
hao wameachiwa huru baada ya kuonekana kuwa hawakubeba dawa za kulevya,
bali kemikali aina ya ephedrine.
Hata hivyo, Mahakama ilibaini kuwa, Melissa hana
hatia kwa kuwa ilionekana kuwa amemsindikiza Masogange, ambaye alimwomba
amsaidie kubeba mzigo huo.
“Mahakama iliona kuwa Melissa aliombwa tu
kumsaidia kubeba baadhi ya mabegi, lakini hayakuwa yake. Mizigo yote
iliandikwa jina la Agness Gerald na si Melissa,” alisema Kapteni
Ramaloko.
Kapteni Ramaloko alisema, Melissa alijitetea kuwa
hakuwa amesafiri pamoja na Masogange bali walikutana ndani ya ndege na
Masogange alimwomba amsaidie kubeba mizigo hiyo, kwani ilikuwa mikubwa.
Kwa sheria za Afrika Kusini kubeba kemikali zozote
ambazo zimepigwa marufuku ni kosa la jinai kisheria, hivyo mahakama
iliamuru Masogange ahukumiwe kwenda jela kwa miezi 30 (miaka miwili na
miezi mitano) au alipe faini ya R30, 000 (sawa na Sh4.8 milioni).
Hata hivyo, Kapteni Ramaloko alisema mdhamini wa Masogange alilipa nusu ya fedha na kwamba zinazobaki amalizie baadaye.
Alisema kutokana na kutomalizia kulipa fedha hizo
ataendelea kubaki nchini humo hadi atakapomaliza kulipa nusu ya faini
iliyobaki.
Masogange na mwenzake walipokamatwa na SARS ilielezwa walikuwa wamebeba dawa za kulevya aina ya
Methamphetamine, lakini Mahakama juzi ilithibitisha walikamatwa na kemikali aina ya Ephedrine, ambayo siyo dawa za kulevya.
Wakati Kamishna Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Dawa
za Kulevya nchini, Geofrey Nzowa alipoulizwa na Mwananchi Jumamosi juzi
alisema mzigo walioubeba Masogange na mwenzake haukuwa ni dawa za
kulevya bali ni kemikali za dawa za kulevya, lakini Msemaji wa Mamlaka
ya Mapato ya Afrika Kusini, (SARS), Marika Muller alieleza kuwa timu ya
SARS ina uhakika kuwa mabegi sita yaliyokamatwa Julai 5 ni dawa za
kulevya aina ya Methamphetamine.
0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII