REGINALD MENGI: MUHONGO NI MUONGO NA MPOTOSHAJI
MWENYEKITI Mtendaji wa makampuni ya IPP, Reginald Mengi
na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, wameingia
katika mzozo mzito kuhusu uwekezaji katika sekta ya gesi.
Katika mzozo huo, Mengi amemshambulia Waziri Muhongo kwa kumwita ni
mwongo, mpotoshaji na mwenye lengo la kuwatoa Watanzania kwenye hoja ya
msingi ya rasilimali yao ya gesi.
Mengi alitoa kauli hiyo jana kupitia taarifa yake aliyoisambaza kwenye vyombo vya habari mbalimbali nchini.
Mzozo wa vigogo hao ulianza wiki mbili zilizopita baada ya Mengi
ambaye pia ni Mwenyekiti wa taasisi ya Uwekezaji nchini (TPSF), kukutana
na waandishi wa habari na kueleza msimamo wa taasisi hiyo katika suala
la uwekezaji wa gesi nchini.
Katika maoni yake, TPSF ilisisitiza umuhimu wa ushirikishwaji wa
Watanzania katika uchumi wa gesi na kuishauri serikali kusitisha ugawaji
wa vitalu vya gesi hadi sera ya gesi itakapokuwa tayari na taasisi hiyo
iliomba kukutana na Waziri Muhongo kwa majadiliano zaidi.
Baada ya ushauri huo, Waziri Muhongo alijibu kupitia vyombo vya
habari kwamba mpango wa kugawa vitalu vya gesi na kuingia mikataba uko
palepale kama ulivyopangwa kufanyika Oktoba mwaka huu.
Prof. Muhongo pia alitamka bila kumng’unya maneno kwamba hana mpango
wa kukutana na TPSF, kwani kufanya hivyo ni kupoteza muda, na kuongeza
kuwa uwezo wa wafanyabiashara wa Tanzania ni kuwekeza kwenye soda na
juisi, si kwenye sekta ya gesi.
Septemba 7, mwaka huu, mzozo huo uliingia katika hatua mbaya zaidi
baada ya mtu aliyejitambulisha kwa jina la ‘CCM Tanzania’, kusambaza
taarifa kwa njia ya barua pepe kwa vyombo vyote vya habari na
kumshambulia Mengi kwa kumwita fisadi, mbinafsi na mfitini wa maendeleo.
TANZANIA DAIMA WANAYO HABARI NZIMA.ENDELEA KUISOMA KWA KUBONYEZA HAPA.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII