P SQUARE WATAPIGIA SHOW HAPA...


Show ya kihistoria inayosubiriwa na wengi kufanyika ndani ya viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam leo, tayari jukwaa litakalotumiwa na wasanii wanne kutoka hapa nyumbani na wale wakali wa kulishambulia jukwaa barani Afrika P~Square lipo katika maandalizi ya mwisho mwisho pamoja na kufunga mziki.

Jukwaa lina sehemu tatu za kupandia juu yaani ngazi na vijukwaa vidogo viwili kama winchi vilivyopo katikati ya stage. Limefungwa sound yenye mjumuiko wa spika zaidi ya sitini.
Wasanii watakao-perform jukwaa moja na P` Square ni Malkia wa Bongo fleva mwenye miaka kumi na tatu kwenye gemu Lady Jay Dee a.k.a Anaconda, King wa R&B Ben Paul, mwamba wa kaskazini Joh Makini na MC shupavu au Heavy weight Mc au Daddy Joseph Haule wa Mitulinga Mchawi wa Rhymes.
CREDIT: VIJIMAMBO BLOG
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII

Copyright © 2013. ArtAfropixels Media.com - All Rights Reserved
Customized by: IT XPERTTZ ONE | Powered by: BS
Designed by: Tilabs