HAWA NDIO MAWAZIRI WANNE WALIOTIMULIWA JANA NA RAIS
RAIS
Jakaya Kikwete amekubali kuwavua vyeo vyao Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,
Shamsi Vuai Nahodha, Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi , Dk David
Mathayo na Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamisi Kagasheki aliyekuwa
tayari ametangaza bungeni kujiuzulu. Taarifa hiyo imetolewa na Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda, bungeni baada ya kueleza kuwa ameongea na Rais na
kukubali kuwavua nyadhifa zao kutokana na ripoti ya Operesheni Tokomeza
iliyosomwa leo bungeni na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi,
Maliasili na Mazingira, James Lembeli.
0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII