UNAMKUMBUKA SHEIKH SHARIFF YULE MTOTO ALIYEZALIWA ANAJUA QURAN? SASA AOKOKA, SOMA HABARI KAMILI HAPA

Yule
 Sheikh Mtoto maarufu kama Sheikh Shariff ambaye aliitingisha Tanzania 
kwa ufahamu mkubwa wa Qur’an akiwa na umri wa miaka tisa hatimaye 
amesalimu amri na kuokoka, katika kanisa la Pentekoste Motomoto jijini 
Dar es Salaam.
Sheikh Shariff ambaye jina lake halisi ni Sheikh Shariff Mohamed Mikidadi tayari amebatizwa na kupewa jina jipya la Michael Sylivester Sewando, ambapo hivi sasa analelewa kiroho katika kanisa hilo lililopo Keko chang’ombe jijini Dar es Salaam.
….Licha
 ya Sheikh Shariff sasa Michael Sewando kuzaliwa katika familia  ya 
kikatoliki ya mzee Sylivester Sewando na mama yake Joyce Mokiwa, alisema
 alisilimu baada ya kutibiwa maradhi yake na mganga muumini wa dini ya 
Kiislamu wakati akiwa mtoto.
Katika
 umri mdogo, jambo hilo lilimfanya ghafla ajikute akianza kuipenda dini 
ya kiislamu na ndipo aliamua kujiunga nayo, ingawaje wazazi wake 
walimpinga vikali.
Alisema
 ilibidi aondoke Nyumbani kwao Kawe Ukwamani na kuhamia kwa ndugu wa 
kiislamu na kuanza kuswali katika msikiti wa Al Shariff, International 
Dawas’ Islamic Centre Kawe Dar es Salaam. (SIDC) alikoingizwa rasmi 
katika dini ya Kiislamu.
Alisema
 mara baada ya kujiunga na dini hiyo na kuanza kuswali katika msikiti 
huo, alijikuta akipata ufahamu mkubwa wa elimu ya Qu’ran pasipo 
kufundishwa. Sheikh Shariff alisema anachojua ni kwamba uwezo wa kuijua 
Qur’an aliupata kutoka kwa majini 2900, yaliyomuingia baada ya kujiunga 
na Uislamu.
Alisema
 majini hayo ndiyo sababu pekee iliyomfanya awe mahiri sana katika elimu
 ya dini ya kiislamu. Akizungumza na wahadhiri mbalimbali nje na ndani 
ya Tanzania huku akifanya miujiza na kuendesha mihadhara mingi ya 
kiislam.
Kwa 
mujibu wa Sheikh huyo aliyeokoka, maeneo aliyowahi kutoa mihadhara ni 
Kawe,Tandika , Mbagala, Njoro, Kilimanjaro, Mwembe tayari nchini Kenya, 
viwanja vya msikiti Mkuu wa Jijini na Kampala nchini Uganda.
Katika
 hali isiyokuwa ya kawaida, Sheikh Shariff alisema aliwahi kuishi chini 
ya bahari ya Hindi katika eneo la Maskati, nchini Oman, akifundishwa 
mambo mbalimbali na majini. Alisema akiwa chini ya bahari alikuwa 
akifundishwa na jini mkuu aliyemtaja kwa jina Lusifa ambalo ni la 
Shetani, ambapo alikuwa akilishwa mchanganyiko wa damu za binadamu na 
wanyama na mifupa ya farasi.
Sheikh
 Shariff au Michael Sewando alisema Lusifa au mkuu wa majini ambaye 
alikuwa na umbo la mfano wa mjusi mkubwa, ndiye aliyemfundisha masuala 
ya uganga wa kienyeji kwa kutumia vitabu maarufu vya kijini. Mambo 
mengine aliyofanyiwa akiwa chini ya bahari ni pamoja na kuwekwa katika 
moto mkali kwa muda wa siku saba na baadaye katika baridi kali na giza 
totoro kwa siku hizo hizo.
Nakumbuka
 nikiwa chini ya bahari ambako naamini ni kuzimu, Lusifa aliamuru kuwa 
kamwe nisilitaje jina la mtu aliyesulubiwa msalabani kwa maana yaYesu, 
kwa vile jina hilo ni baya na huharibu kazi za kuzimu. Pamoja na mambo 
mengine mengi ya ajabu aliyofanyiwa au kufundishwa na Lusifa, alisema 
baadaye alihitimu na kupatiwa mikoba mitatu iliyosheheni madawa ya 
mitishamba, viungo vya wanyama, binadamu na majoka. Unajua nilikuwa 
nafanya masuala ya kuagua watu kiganga huku pia nikiendesha mihadhara 
mbalimbali ya kiislamu’’ alisema akionyesha kitambulisho kinachoonyesha 
kuwa ni mganga wa kienyeji.
Alisema
 katika shughuli zake aliwahi kuwasilimisha wakristo mbalimbali wakiwepo
 mapadri na wachungaji, ambapo ameahidi kuwarudisha kwa Yesu baada ya 
kuokoka. Aidha alibainisha kuwa aliwahi kuoa majini mawili na 
kusababisha ajali zilizopoteza maisha ya watu ili kupata damu na nyama 
za majini aliyokuwa akiyamiliki.
Kuhusu
 jinsi alivyokutana na Yesu na kuokoka, alisema hivi karibuni wakati 
akielekea katika shughuli zake za uganga eneo la Mbagala Mgeni Nani, 
miguu yake ghafla ilinasa ardhini na akasikia sauti ya Yesu ikimwambia 
kwamba aachane na uchafu wake, ili atakaswe kwa damu yake Yesu lakini 
alitaka kupinga.
Alisema
 akiwa katika hali ya kupinga sauti hiyo, alitokea mama mmoja aliyekuwa 
muislam lakini akaokoka, ambaye alimshauri aokoke na kumuongoza zaidi 
hadi katika kanisa la Pentekoste Motomoto lililoko Keko Chang’ombe 
alikomkiri Yesu na kuokoka baada ya kutolewa mapepo. Kanisa la 
Pentekoste Motomoto linaongozwa na Mchungaji Ibrahimu John ambaye kwa 
sasa ndiye baba wa kiroho wa Sheikh Shariff.
Sheikh
 Shariff (Michael Sewando) alisema baada ya kuokoka, amekuwa akipata 
mashambulizi kutoka kwa majini na wachawi hivyo anaomba msaada wa maombi
 kutoka kwa wacha Mungu wote.
SOURCE: MSEMA KWELI
 
 
 
 

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
Karibu kwa Yesu Michael, usiogope, Bwana anasema kwenye LUKA 10:19 Nimewapa mamlaka ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitakachowadhuru.
ReplyDeleteAmini kwamba wewe ni zaidi yao katika Jina la Yesu Kristo aliyekuokoa kutoka kwenye himaya yao Yeye atakutegemeza na kukulinda kwa kila mshale wa kuzimu
Anasema kwenye EBRANIA 12:29 Mimi ni MOTO ULAO
Mungu mwenyewe ajiwekaye kwenye umbo la moto akushukie na kuteketeza kila kikutesacho kwa Jina la Yesu Kristo na ufunikwa kwa damu yake iliyomwagika msalabani kama asemavyo kwenye UFUNUO 12:11 Nao wakamshinda shetani kwa damu ya Yesu.
Amen.
Muhuni huyo hana lolote anatafuta maslahi ya kifedha.
ReplyDeleteAmen
ReplyDeleteDuniani kuna mambo hyo siku ya mwisho sidhani kama kuna mtu atapona kwa %100
ReplyDeletemi yamgu macho
ReplyDelete