Aunt Ezekiel Ajutia Kitendo Alichokifanya Fiesta

MSANII wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel amesema kuwa anajutia matukio ya aibu aliyoyafanya hivi karibuni ya kuanika nyeti zake hadharani kwani yamemfanya ajishushie heshima. Akizungumza na Gazeti la Ijumaa, Aunt alisema kitendo cha kupanda jukwaani na kucheza kihasara kiasi cha kuonesha sehemu zake nyeti akiwa mkoani Tanga na Mwanza kwenye Tamasha la Fiesta kilisababishwa na pombe alizokuwa amegida.

“Kwa kweli zilikuwa ni pombe tu, najuta lakini naamini hali ile haitajirudia tena,” alisema Aunt. Akizungumzia madai kwamba alipokuwa jukwaani mkoani Mwanza alijikojolea na kuifanya nguo aliyoivaa iloe, Aunt alisema: “Nimeshangaa kudaiwa kuwa nilijikojolea, ukweli ni kwamba sikufanya hivyo, nilianguka nikakalia maji ndiyo maana ikawa vile.”
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

2 comments:

  1. Sidhani kama inamuumiza sana ni kwa kuwa tu watu wamemlalamikia otherwise kwake ni kawaida tu kukaa uchi hovyo. Kwani muvi ngapi anacheza nusu uchi iyo ya kuwa jukwaani ndo aombe radhi na kujuta!!? She can not be serious!

    ReplyDelete
  2. Muwaombee dada zenu jaman, wanahisi wakifanya upuuzi ndo umaarufu utaongezeka....

    ReplyDelete

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII

Copyright © 2013. ArtAfropixels Media.com - All Rights Reserved
Customized by: IT XPERTTZ ONE | Powered by: BS
Designed by: Tilabs