Showing posts with label bongomovie. Show all posts

MAMA KANUMBA AOMBA WADAU WAMSAIDIE

0 comments

MAMA wa msanii nguli wa filamu nchini marehemu ‘Steven Kanumba’ Frola Mtegoa amesema yuko katika mkakati wa kuandaa filamu inayohusu maisha ya mwanaye kiasi cha kufikia hatua ya kuomba msaada ‘kutembeza bakuli’.
Mama mzazi wa marehemu ‘Steven Kanumba’ Frola Mtegoa.
Akizungumza na paparazi wetu mama huyo alisema kwamba, anapata wakati mgumu kukamilisha jambo hilo kutokana na kukwama na kutaka asaidiwe ili kufanikisha jambo hilo.
“Nimekwama na nawaomba wadau wajitokeze kunisaidia nikamilishe hili, nahitaji msaada wa kifedha na hata ushauri,”alisema.
Mama huyo alisema lengo la kuandaa kazi hiyo ni kutaka kufikisha ujumbe katika jamii kwa kuamini kwamba wengi watajifunza kupitia maisha ya mwanawe.
Marehemu Steven Kanumba.
Amemtaka yeyote ambaye atakayeguswa na jambo hilo asisite kuwasaliana naye na kumsaidia.

                                                                            GPL

Soma zaidi Hapa »

WASANII 10 WA KIKE WA BONGOMOVIE WALIOFANYA VIZURI ZAIDI MWAKA HUU NDIO HAWA

0 comments
Hii ni orodha ya waigizaji wa kike nchini waliofanya vizuri mwaka 2013. Orodha imeandaliwa   kwa msaada mitandao inayoandika habari za filamu nchini, wadau mbalimbali wa filamu pamoja na makampuni ya kusambaza filamu nchini.

SHAMSA FORD.
  Shamsa_ford2
Shamsa amefanya poa sana mwaka huu katika filamu nyingi. Katika filamu ya ‘Bado Natafuta’ ameonyesha uwezo wake na kuwavutia wengi.Filamu nyingine alizofanya kwa mwaka huu ni Shikamoo Mzee,Zawadi Yangu pamoja na Impossible.


IRENE PAUL. 


  Irene-Bahati-Paul-cut
Irene ni mmoja ya msanii wa filamu ambao ameoneka kukubalika sokoni. Mwaka 2013 ametamba katika filamu ya Majuto na Best Losers,Fiona,Chinga Codineta, Love & Power, Kalunde zingine.


RIYAMA ALLY.

  RIYAMA-ALLI-CUT
Riyama mwaka huu ametamba na filamu kama Nimekuchoka, King’amuzi, Nipe Ripoti, My Enemy, Magata, Kovu La Siri ambazo zimemfanya mwaka huu aonekane ni mmoja wa waigizaji waliofanya vizuri 2013.


JACKY WOLPER  wolper-1
Jacky ni msanii wa filamu ambaye kwa mwaka huu amefanya filamu kama After Death,Crazy Desire,Mbegu, Pain for Pain P.F.P na nyingine nyingi. 


JOHARI 
clip_image001_thumb[2]
Johari ni mmoja wa wasanii wa filamu wa kike waliofanya kazi nyingi na marehemu Steven Kanumba lakini mpaka leo bado uwezo wake ni mzuri.Mwaka huu Johari amefanya filamu kama Mr. Masumbuko, Bad Luck, Rudi Kaburini, Vagabond na zingine.


YVONNE CHERRYL(MONALISA)  

  Yvonne-Cherryl-Monalisa-480x511
Mwanadada huyu bado anaendelea kufanya vizuri kadri siku zinapozidi kwenda.Mwaka huu amefanya filamu kama Daladala, Mwisho Wa Siku na pia kung’ara kwenye tamthilia ya ‘Siri Ya Mtungi’ iliyotajwa kuwania tuzo saba za Africa Magic.


ELIZABETH MICHAEL(LULU)  Lulu
Pamoja na kutoa filamu chache mwaka huu, Lulu ni msanii wa filamu maarufu zaidi baada ya Wema Sepetu. Mwaka huu ametamba na filamu yake ya Foolish Age ambayo ilifanya vizuri sokoni.

CATHY RUPIA 

  CATHY RUPIA
Cathy ni mmoja kati ya waigizaji wazuri. Mwaka huu amefanya filamu kama Melvin, Bad Luck, Pain Killer, Zulfa,Without Daddy, Nesi Selena na zingine.


 

AUNT EZEKIEL

  AUNT EZEKIEL
Mwaka huu ametamba na filamu kama Scola, Prison Revenge,Last Step,Pumba,Radio Presenter pamoja na nyingine nyingi.

WASTARA JUMA   wastara
Ni mwigizaji wa siku nyingi sana,kwa mwaka huu ameonyesha kufanya vizuri katika filamu kama Kivuli ana Shaymaa ambazo zipo sokoni kwa sasa.

Soma zaidi Hapa »

MOVIE MPYA YA BABA MADAHA, TAZAMA TRAILER YAKE HAPA

0 comments
Mwanadada anayefanya mambo mengi sana kwenye muziki na filamu Baby Joseph Madaha anatarajiwa kufanya uzinduzi wa filamu yake mpya ya The Gal Bladder hapo kesho kwenye ukumbi wa mgahawa wa Akemi jijini Dar es Salaam.




Baby Madaha amesema kuwa uzinduzi huu utahusisha waalikwa tu na sio wa viingilio kama ilivyozoeleka kwenye uzinduzi wa vitu mbalimbali hapa nchini.


Tazama Trailer yake Hapa Chini


Soma zaidi Hapa »

KIOJA CHA MWAKA, TAZAMA VIDEO HII YA MAITI ILIYOGOMA KUSAFIRISHWA

0 comments




Jiji la Eldoret kaunti ya Uasin Gishu nchini Kenya leo lilishuhudia tukio la kushangaza baada ya maiti iliyokuwa inasafirishwa kwa maziko kukataa safari hiyo.

Kizaazaa kilizuka pale gari lililokuwa limelibeba jeneza lenye mwili wa marehemu kupata hitilafu na licha ya kubadilishwa gari jingine, nalo pia lilikataa kuwaka. 

Hapo ndipo marafiki na jamaa ya marehemu walipochukua fursa ya kuirai maiti hiyo ili ipate kufikishwa eneo la maziko. 

Baada ya maombi ya takribani saa moja kutoka kwa ndugu na jamaa wa marehemu kuiomba maiti hiyo ikubali kusafirishwa, hatimaye safari ilianza na kuacha maswali mengi yasiyo na majibu kwa mashuhuda wa tukio hilo.

Soma zaidi Hapa »

HAHAHA!! BOFYA HAPA, UTACHEKA MPAKA UKAE CHINI

0 comments




Soma zaidi Hapa »

DR CHENI AMPA SHAVU MCHINA KATIKA MOVIE YAKE, MCHINA ASEMA BIASHARA NGUMU BORA AIGIZE...BOFYA HAPA

0 comments
Dr. Cheni amleta Mchina Bongo Movies. Mwenyewe adai biashara ngumu acha ajaribu fani
Baada ya kumuingiza shabiki maarufu wa yanga football club “Steven” sasa Dr Cheni afanya mabadiliko makubwa ya bongo movie baada ya kumuweka mchina kwenye movie yake mpya.

Moja ya scenes ambazo mchina huyo amecheza ni sehemu ambayo amefumaniwa akiwa Guest. 

Tuliamua kumtafuta Mchina huyo Mr. Chaoxiang Deming ( 朝翔 德明  ) kujua kwanini kwanini amemua kujiingiza kwenye tasnia ya filamu nchini na alidai kuwa kwa sasa biashara imekuwa ngumu kidogo hivyo sio mbaya akajaribu kufanya mambo mawili matatu kuongeza kipato

Tazama scene hiyo alizoigiza mchina huyo  AKIWA AMEFUMANIWA GESTI

Soma zaidi Hapa »

WOLPER : 'SIKUFUATA PESA KWA DALAS, PESA NILIKUWA NAYO NA NINAYO MPAKA SASA'

0 comments
 STAA wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper amefunguka kuwa suala la yeye kuachana na aliyekuwa mpenzi wake, Abdallah Mtoro ‘Dallas’ halikusababishwa na ukata kwani yeye hakufuata fedha kwa mwanaume huyo.
Jacqueline Wolper.
Akijibu swali la paparazi wetu lililomtaka afunguke kama alifuata mkwanja kwa Dallas, Wolper alisema moyo wake huwa hauna tamaa ya fedha na aliingia katika penzi la Dallas kwa mapenzi aliyokuwa nayo wakati huo na kwa kuwa yaliisha, maisha yanaendelea.
 
Abdallah Mtoro ‘Dallas’.
“Sikufuata pesa kwa Dallas, pesa ni pesa na mapenzi ni mapenzi. Kama ni pesa nilikuwa nazo na hata kabla sijawa naye na sasa pia ninazo, waniache,” alisema Wolper.
SOURCE : GPL

Soma zaidi Hapa »

ULISHAIONA ILE VIDEO YA BABY MADAHA ILIYOZUA 'UTATA'??? BOFYA HAPA UITAZAME

0 comments
Video mpya ya baby Madaha “Squeeze me tight” yazua utata, tazama hapa
Video ya muziki ya mwanadada Muigizazji na mwanamuziki Baby Madaha “Squeeze me tight” imeanza kuzua utata kwenye mitandao ya kijamii baada ya kutazamwa na watu wengi sana kwa muda mfupi tangu ilipowekwa hewani kwenye mtandao wa youtube.
Video hiyo ambayo imerekodiwa huko nchini Kenya chini ya Studio za Candy n’ Candy Records ina mahadhi ya kijamaika flani hivi  na pia ukiichunguza kwa umakini zaidi ina vionjo flani vya “kizombie” na pia ipo “too sexy” kitu kilichotafsiriwa kama mambo yale  ile “dini ya wavaa suti” na sababu ya video hii kutazamwa sana. Tuliamua kumtafuta baby Madaha mwenyewe ili ajibu tuhuma hizi lakini kwa bahati mbaya simu yake ya mkononi likuwa inatumika muda wote tuliompigia. Tutaendelea kumtafuta na kuwajulisha atakayosema.
BONYEZA HAPA KUITAZAMA

Soma zaidi Hapa »

VAN VICKER KUIGIZA MOVIE NA WABONGO, HASHIMU KAMBI AELEZEA UJIO WAKE.....SOMA ZAIDI

0 comments

v
Van Vicker muigizaji kutoka Ghana ambaye anafanya vizuri hadi nchini Nigeria ameingia Tanzania jumapili iliyopita na anaondoka leo tarehe 19/9 kurudi kwao Ghana. Hashimu Kambi ambaye ndiyo mwenyeji wake akiongea na millardayo.com alisema,”Van Vicker amekuja Tanzania kuigiza movie yangu ambayo mwanzoni niliipa jina la The Network. Lakini kutokana na kuwa kuna movie nyingine ambayo imetoka na jina hilo hilo nimeamua ku-change jina. Hadi sasa nina majina manne bado sijaamua kutumia lipi.”
Hashimu Kambi aliendelea,”Vicker amefika hapa Tanzania jumapili na anamalizia baadhi ya scene leo na ataondoka leo usiku tare 19/9. Kazi ikiwa tayari tutawaambia inavyotoka na watanzania wasubili kitu kizuri kwasababu kwenye hii movie kuna watu kama Vicker mwenyewe,Weru Sengo,Irene Paul na wengine. So, itakuwa kazi nzuri sana”
Van vicker  anaonekana kufurahia kuwa Tanzania kwasababu amekuwa akipiga picha sehemu nyingi sana anazokuwa.vicker3
vq
vq2
1d

Soma zaidi Hapa »

WEMA SEPETU NAYE AJA NA TV SHOW YAKE, KUONYESHWA EATV.....SOMA HAPA

0 comments
kipindi cha Wema kuanza kuruka hewani kwenye kituo cha TV cha EATV kuanzia mwezi ujao
Kile kipindi cha Reality Show ya maisha ya mwigizaji Wema wepetu ambacho hapo mwanzo kilipangwa kuanza kuoneshwa na kituo cha TV cha Clouds cha jijini Dar es salaam, sasa kitaanza kuonekana kwenye kituo cha EATV kuanzia mapema mwezi ujao.
Kwa mujibu wa taarifa za mtandao toka kwenye kituo hicho cha TV ambazo hazijaelezea sababu hasa za kipindi hicho kuamia kwenye luninga hiyo zinasema kuwa, fans wa mwanadada hyuo wake tayari kwa ajili ya show hiyo ya kwanza na aina yake bongo.

Soma zaidi Hapa »

TAZAMA VIDEO MPYA YA HAMMER Q NA MKEWE SALHA

0 comments
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiphY7xo6pSQNUupaIFVcJ4kwfhEQdU9G8Py8jK9u4ar5heGaeEBHeXIcVz36bkuvkQu6slI03ZmoFopfD-YBAPOWKUI9K949Bj7IV0PoSpM3TjFgzIUeWwjAVLY8arUZ9L4L_tP1sOA9Iz/s640/ha.jpg


Soma zaidi Hapa »

NEW VIDEO : FEZA KESSY - AMANI YA MOYO

0 comments
 
Ni video mpya ya mwanadada Feza Kessy ambae kwa sasa yupo ndani ya shindano la Big Brother Africa; The Chase ambalo hufanyika kila mwaka mara moja akiiwakilisha Tanzania
Pamoja na kuwa mshiriki kwenye jumba hilo, Feza pia ni msanii wa muziki, hadi sasa ameshatoa ngoma yake inayokwenda kwa jina la “AMANI YA MOYO”… Na hii ndiyo video ya ngoma hiyo ambayo Director Nisher (Arusha) ametisha tena kwa utengenezaji wake … Recently Nisher amefanya video kali ya Ben Pol – Jikubali …
Check AMANI YA MOYO hapa chini….


Soma zaidi Hapa »

HII NDIO VIDEO MPYA YA BEN POL- JIKUBALI....ITAZAME HAPA NOW

0 comments


Soma zaidi Hapa »
Copyright © 2013. ArtAfropixels Media.com - All Rights Reserved
Customized by: IT XPERTTZ ONE | Powered by: BS
Designed by: Tilabs