Showing posts with label mchanganyiko. Show all posts

MAMBO YA MSWATI NDIO HAYA.....DUHH

0 comments

Baadhi ya Wasichana vigori wa Swazland wakiwa kwenye gwaride rasmi tayari mmoja wao kuchaguliwa na King Mswati 11 kuwa mke wake. Mchakato huo hufanyika kila mwaka.
Once described as the ‘luckiest man’ in Africa, Swaziland’s King Mswati III picked an 18 year-old beauty contestant as his 14th wife, revealed a palace spokesman.
“I can confirm that the king has introduced to the nation a new liphovela (royal fiancee),” said Timothy Mtetwa, the palace governor.
Young Swazis participate in the Reed Dance. [photo/mobile.saharareporters.com ]
Young Swazis participate in the Reed Dance. [photo/mobile.saharareporters.com ]
The King is said to have ‘noticed’ the 18-year-old former high school student who graduated last year in the Reed Dance ceremony held last month. The Reed Dance is an annual traditional Swazi dance ceremony where young Swazi women parade past the king, bare-chested, to allow the King to pick a new wife. The ceremony has become a tourist sensation in the small landlocked southern African country as sometimes tourists join the dance ‘just for the fun of it’. In may, a 15-year old student at a local private school near the residence palace of the king’s fourth wife fled to Britain after the king begun making advances at her to join the harem of his then 13 wives.
“No one ever says no to the King, so I just fled when he begun contacting my school,” the girl had indicated then. It took the intervention of the aunt who smuggled her out to Britain to continue with her education.
King Mswati. [photo/telegraph.co.uk]
King Mswati. [photo/telegraph.co.uk]
The new bride, Sindiswa Dlamini, whom the King picked last month, was introduced to the royal household adorned in red feathers after it was found expectant. It is a tradition that the King’s virgin pick must become pregnant before joining the country’s royalty.

About NOMAD from SleepOut.com

Travel just like life should be inspiring, amusing, down-to-earth and diverse. NOMAD brings together original travel pieces by SleepOut.com guests and writers from around the globe written expressly for the NOMAD in you.












Soma zaidi Hapa »

TAZAMA PICHA ZA MABASI YA MWENDO KASI YALIPOKUWA YAKIFANYIWA MAJARIBIO LEO MITAANI

0 comments


Mmoja ya basi la mwendo kasi likikatiza mtaa wa Lumumba ikiwa sehemu ya majaribio ya mabasi hayo ambayo yanaaminika yataondoa kabisa tatizo la usafiri katika jiji la Dar es Salaam.
CREDIT : GPL

Soma zaidi Hapa »

SHILOLE AMUANIKA MCHUMBA AKE WA KIZUNGU, TAZAMA PICHA NA SOMA ALICHOKISEMA

0 comments
KWA mara ya kwanza msanii wa filamu na muziki Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amenaswa akiwa na mwanaume wa Kizungu anayedaiwa kuwa ndiye mchumba wake.
Zuwena Mohamed ‘Shilole’ akiwa na mchumba wake.
Chanzo makini kimepenyeza habari kuwa, safari za mara kwa mara za Shilole nchini Uingereza zimekuwa zikisababishwa na mchumba huyo wa Kizungu ambaye huwa anamuita kufurahia penzi lao pamoja na kumtafutia shoo mbalimbali.
“Ukweli ni kwamba Shilole ana mchumba wa Kizungu na walikutana kwenye shoo ya mara ya kwanza aliyoenda kufanya nchini Uingereza na hivi karibuni ataenda tena na amealikwa na huyo mchumba wake,” kilisema chanzo hicho.
Gazeti hili limekuwa la kwanza kunasa picha kadhaa za Shilole akiwa katika mapozi tofauti ya kimahaba na Mzungu huyo.
Baada ya chanzo hicho kumwaga ‘upupu’ huo, mapaparazi wetu walimtafuta Shilole ili aweze kufunguka ambapo bila kuumauma maneno, alikiri kuwa amepata mchumba huyo aliyemtambulisha kwa jina la Ankar.
Akizidi kumwaga data za boifrendi wake huyo, Shilole alisema awali walikutana kwenye moja ya shoo zake nchini humo ndipo urafiki ulipoota mizizi na kufikia hatua ya kuwa wapenzi.
“Kweli nina mchumba Mzungu ambaye ni raia wa Uingereza, nilipokuwa napataka nimefika, sipindui tena. Unajua muziki wangu na mauno yangu yanawavutia sana watu, siku ya kwanza aliniona kwenye shoo akanipenda ndipo tukaanzisha urafiki.
“Hivi karibuni nina safari ya kwenda nchini humo kwa mwaliko maalum alionipa, nitaenda peke yangu kwani safari nyingine zote zilizopita nilikuwa naenda na watu,” alisema Shilole.

Soma zaidi Hapa »

HIVI NDIVYO M4C ILIVYOKULA VICHWA MOROGORO, AFANDE SELE NAYE ALIHUTUBIA

0 comments

Halima Mdee: Mbunge wa Kawe, Halima Mdee akiwahutubia maelfu ya wakazi wa mji wa Mtibwa, katika mkutano wa Operesheni M4C Pamoja Daima, uliofanyika jana.
Mbowe na Afande Sele: Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akimtambulisha mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya, Afande Sele, wakati wa mkutano wa Operesheni M4C Pamoja Dama, uliofanyika katika Kata ya Tungi mjini Mororgoro jana.
Afande Sele: Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya, Afande Sele akiwahutubia wananchi wa Kata ya Tungi mjini Morogoro jana, katika mkutano wa hadhara wa Operesheni M4C Pamoj Daima, ambao pia ulihutubiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe.
Mbowe, Halima wakiondoka Ifakara: Mwenyekiti wa Chama cha Demokreasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee wakiondoka baada ya kuhutubia mkutano wa Operesheni M4C Pamoja Daima, uliofanyika mjini Ifakara jana.
Mkutano Ifakara: Maelefu ya wakazi wa mji wa Ifakara, wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa Operesheni M4C Pamoja Daima, ambao ulihutubiwa na Mweneyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) jana.
Mabango Ifakara: Baadhi ya wananchi mji wa Ifakara wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe mbalimbali, wakati wa mkutano wa Operesheni M4C Pamoja Daima, ambao ulihutubiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe jana.

Wananchi Ifakara: Sehemu ya maedlfu ya wakazi wa mji wa Ifakara, wakitawanyika baada ya mkutano wa Operesheni M4C Pamoja Daima, ambao ulihutubiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe jana.
(Picha na JF)

Soma zaidi Hapa »

KIOJA: MCHUNGAJI AFA MAJI BAADA YA KUJARIBU KUTEMBEA JUU YA MAJI KAMA YESU, SOMA HAPA

0 comments
NIGERIA. Ilikuwa sikitisho kubwa kwa waumini baada ya mchungaji wao kusombwa na maji baada ya kujaribu kutembea juu ya maji kama vile masihi Yesu alivyofanya wakati wake alipokuwa duniani.

Pastor Frank Kabele mwenye umri wa miaka 35, aliwaambia waumini wake kuwa mtu mwenye imani anaweza kufanya miujiza yeyote ila tu uwe na imani. Aliwaahidi wafuasi wake kuwa atatembea juu ya maji pindi tu atakapomaliza maombi yake.

Lakini mambo yalienda ndivyo sivyo baada ya pastor huyo kujaribu kutembea katika mto mkubwa, alididimia mtoni humo na ilikuwa vigumu kwa waumini wake kumsaidia kwani maji yalikuwa na nguvu nyingi

Soma zaidi Hapa »

VERY SAD!! MFANYABIASHARA WA KIKE AUAWA KWA KUPIGWA RISASI NA MAJAMBAZI KARIAKOO, TAZAMA PICHA HAPA

0 comments
TUNAOMBA RADHI KWA PICHA
 Mwili wa mfanyabiashara huyo ukiwa kwenye gari mara baada ya kupigwa risasi na majambazi (majira ya saa 12 Kasoro jioni)
 Damu ya Mfanyabiashara huyo ikiwa imetapakaa katika gari lake baada ya kupigwa risasi na majambazi waliompora kiasi kikubwa cha fedha na kutoweka.
Raia wakishangaa mwili wa mfayabiashara huo ukiondolowa na polisi
Askari wakiliondoa gari la mfanya biashara huyo katika eneo la tukio
EFD machine ikiwa katika gari la mfanyabiashara aliyepigwa risasi leo jijini Dar es Salaam
Sehemu  ya fremu inayosemekana kuwa ni Duka la mfanyabiashara aliyepigwa Risasi Leo majira ya saa 12 jioni

Mfanyabiashara mmoja (Jina Halikufahamika) Mwenye asili ya Asia ameshambuliwa na majabazi (majira ya saa 12 Kasoro jioni )kwa kupigwa risasi katika paji la uso wake na kisha majambazi hao kutoweka na mabegi mawili yaliyoojaa fedha.
Hata hivyo haikujulikana kwa haraka ni kiasi gani cha fedha ambacho kilikuwemo katika mabegi hayo. Wakiongea na mwandishi wetu baadhi ya mashuhuda wa tukio walidai kuwa majambazi hao walikuwa  watatu na mmoja alikuwa na bunduki aina ya SMG. 
Wakielezea tukio hilo baadhi ya wafanyabiashara wengine katika maeneo hayo ya mtaa wa Lindi na Kongo (Kariakoo) walidai kwamba Mfanyabiashara huyo alitoka na kufunga duka lake huku akiwa na mabegi mawili na Mashine ya kutolea Risiti ya EFD na kuelekea katika gari lake dogo aina ya Suzuki Carry na Ghafla walitokea watu wawili waliokuwa katika pikipiki na mmoja wa tatu alikuwa amesimama pembeni kidogo na gari hiyo na kisha kuelekea moja kwa moja katika gari hiyo na kumpiga risasi mfanya biashara huyo aliyekuwa akijiandaa kuondosha gari lake.
 'Niliona watu kama wanagombania begi hivi ghafla nikasikia mlio wa risasi  na kisha nikaona pikipiki mbili aina ya boxer zikija kwa kasi kutokea upande wa mtaa wa gerezani na kisha  mlio wa pili wa risasi ulikika tena, nahisi ndio uliokuwa umemlenga yule "muhindi" na baada ya hapo kitendo kama cha dakika mbili hivi wale jamaa wakapokezana lile begi na kisha kupiga risasi nyingine juu basi hapo wote tukaanza kufunga maduka yetu na wale majambazi wakatoweka kirahisiii"
Hata hivyo baadhi ya watu wamelaumu utaratibu wa wafanya biashara wengi wa kariakoo kuhifadhi fedha nyingi katika maduka na badala yake wamewataka wafanya biashara hao kutafuta mbinu mbadala itakayowaezesha kuweka fedha na mali zao salama kabisa ikiwa ni pamoja na kutumia huduma za kuhamisha fedha kwa kutumia mitandao, cheque, na hata credit card kuliko Cash kwani imekuwa kawaida kwa mtukio haya kujirudia eleo hili la Kariakoo.

CREDITS TO JG

Soma zaidi Hapa »

KWELI HUJAFA HUJAUMBIKA, TAZAMA PICHA ZA HUYU KIJANA ANAYETESEKA NA UGONJWA WA AJABU

0 comments
 KIJANA Haruni Kayombo (19), mkazi wa Mbalizi, Mbeya anaishi kwa mateso makubwa tangu mwaka 2006, baada kushikwa na ugonjwa wa ajabu uliomuanza ghafla.
Haruni Kayombo.
Katika mahojiano na gazeti hili akiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam, Kayombo alisema bado hajui hatima ya maisha yake kutokana na mateso anayoyapata usiku na mchana huku akitoa simulizi ya majonzi namna gonjwa hilo lilivyomtokea.
Alisema awali akiwa na umri wa miaka 11 alilazwa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya lakini baadaye wazazi wake walifariki dunia na hakupata kuwajua ndugu zake jambo ambalo anaona hakuna haja ya kuwa binadamu huku akionekana mwenye mateso makubwa.
“Sioni faida ya kuwa binadamu, niliugua kama utani, ilifika wakati nikajua kitu cha kawaida, nilishangaa kuona linazidi kuongezeka nilijua utakuwa ugonjwa wa muda mfupi,  lakini nikashangaa usiku na mchana mateso yanazidi.
“Ni tatizo ambalo hata mimi mwenyewe sijui chanzo chake, lilianza kama kauvimbe ka kawaida, sikutambua mapema na sikuwa na hela kwenda kwenye kituo cha afya kwa matibabu zaidi.
“Nilijipa moyo kuwa ipo siku nitakuwa sawa lakini kwa mpaka sasa nimeshakata tamaa, sina baba wala mama, hapa kweli kuna haja ya mimi kuitwa binadamu? Sina kazi na sikubahatika kusoma ni nani atakayeokoa maisha yangu?
“Maisha haya ni Mungu tu anayeweza kuniokoa, inaniuma sana! Ningekuwa na ndugu wangeweza kunisaidia japo hata pesa ya matumizi. Eee... Mola okoa maisha yangu (analia). Napenda kuishi kama binadamu wengine lakini kwa hali hii sina amani kabisa.
“Zamani wakati tatizo linaanza nilikuwa na tabia ya kusali mara kwa mara lakini nimefika hatua ya kukata tamaa na kuona hakuna haja.
“Namuomba rais aje anitembelee ajionee mateso ninayoyapata usiku na mchana, nimepangiwa kwenda kufanyiwa operesheni India lakini sijui lini na itakuwaje!” alisimua Kayombo na kumaliza na kilio tena.
Kama utakuwa umeguswa na tatizo la Haruni Kayombo basi usisite kutoa mchango wako kwenye namba yake ya simu, mtumie kwa njia ya M-PESA ama wasiliana naye moja kwa moja akiwa ndani ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa namba +255764548607.

GPL

Soma zaidi Hapa »

PICHA ZA MWANADADA JACK CLIFF (MUUZA SEMBE) AKIWA KATIKA POZI TOFAUTI ZIPO HAPA

1 comments





Soma zaidi Hapa »

PICHA : LIONEL MESSI ALIPOZULU TANZANIA ..

0 comments






SHUKA CHINI KUTOA MAONI YAKO
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI


Soma zaidi Hapa »
Copyright © 2013. ArtAfropixels Media.com - All Rights Reserved
Customized by: IT XPERTTZ ONE | Powered by: BS
Designed by: Tilabs