CCK yaitaka Chadema iache ubabe
CHAMA cha Kijamii (CCK), kimekijia juu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kukitaka kitafakari kiini cha matukio ya mauaji yanayotokea katika mwendelezo wa siasa zake.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa CCK, Renatus Muabhi, alisema ubabe na kauli zinazotolewa na katibu mkuu wa chama hicho, Dk. Willbrod Slaa, zinaweza kuhatarisha usalama wa nchi.
“Kwa kusimamia misingi na maadili, tunapenda kukiasa Chadema kukaa na kutafakari misingi na chanzo cha matatizo yanayokinyemelea, yakiwamo ya wananchi kuuawa katika mikutano yake,” alisema na kuongeza:
“Tunajua na ni ukweli usiopingika kwamba Chadema ni chama ambacho kimejizolea umaarufu mkubwa kiasi cha kuwa tishio kwa chama tawala (CCM). Tabia ya kuwafanya wananchi kuwa kuni za kuchochea siasa chafu iachwe, kwa kuwa wao ndio wanaoteseka na si wanasiasa.
“Chama hiki kimejengwa kwa hali na mali katika mazingira magumu kufikia kilipo hivi sasa, hivyo ni jukumu lao kujitathimini na kutafuta mbinu mpya ya kukwepa siasa hatarishi, ili kufikia azma sahihi,” alisema.
Aliongeza kuwa ubabe na kauli za Dk. Slaa, ikiwamo ya kumtumia ujumbe mfupi wa maneno Mkuu wa Jeshi la Polisi chini, Said Mwema kwamba aandae risasi nyingi ili wakauwe raia haipaswi kufumbiwa macho, kwani inatengeneza kizazi kisicho na utii wa sheria.
Mbali ya kuzungumzia mwenendo wa hali ya kisiasa nchini, Muabhi aliigeukia Serikali na kusema kuwa imeshindwa kusimamia huduma za kijamii na badala yake imejikita katika mbinu chafu za kuzuia hoja za kuikosoa kupitia mijadala na mikutano inayofanywa na vyama vya siasa.
“Hatusemi ni bahati mbaya kwa kuwa mauaji yaliyotokea Septemba 2, mwaka huu ya mwandishi wa habari Daudi Mwangosi, inaonekana kabisa yalifanyika kwa makusudi, jambo ambalo linaonyesha kuwa Serikali imejipanga kufifisha demokrasia kwa njia ya mtutu wa bunduki,” alisema. TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa CCK, Renatus Muabhi, alisema ubabe na kauli zinazotolewa na katibu mkuu wa chama hicho, Dk. Willbrod Slaa, zinaweza kuhatarisha usalama wa nchi.
“Kwa kusimamia misingi na maadili, tunapenda kukiasa Chadema kukaa na kutafakari misingi na chanzo cha matatizo yanayokinyemelea, yakiwamo ya wananchi kuuawa katika mikutano yake,” alisema na kuongeza:
“Tunajua na ni ukweli usiopingika kwamba Chadema ni chama ambacho kimejizolea umaarufu mkubwa kiasi cha kuwa tishio kwa chama tawala (CCM). Tabia ya kuwafanya wananchi kuwa kuni za kuchochea siasa chafu iachwe, kwa kuwa wao ndio wanaoteseka na si wanasiasa.
“Chama hiki kimejengwa kwa hali na mali katika mazingira magumu kufikia kilipo hivi sasa, hivyo ni jukumu lao kujitathimini na kutafuta mbinu mpya ya kukwepa siasa hatarishi, ili kufikia azma sahihi,” alisema.
Aliongeza kuwa ubabe na kauli za Dk. Slaa, ikiwamo ya kumtumia ujumbe mfupi wa maneno Mkuu wa Jeshi la Polisi chini, Said Mwema kwamba aandae risasi nyingi ili wakauwe raia haipaswi kufumbiwa macho, kwani inatengeneza kizazi kisicho na utii wa sheria.
Mbali ya kuzungumzia mwenendo wa hali ya kisiasa nchini, Muabhi aliigeukia Serikali na kusema kuwa imeshindwa kusimamia huduma za kijamii na badala yake imejikita katika mbinu chafu za kuzuia hoja za kuikosoa kupitia mijadala na mikutano inayofanywa na vyama vya siasa.
“Hatusemi ni bahati mbaya kwa kuwa mauaji yaliyotokea Septemba 2, mwaka huu ya mwandishi wa habari Daudi Mwangosi, inaonekana kabisa yalifanyika kwa makusudi, jambo ambalo linaonyesha kuwa Serikali imejipanga kufifisha demokrasia kwa njia ya mtutu wa bunduki,” alisema.
0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII