Chelsea yaiburuza Arsenal kwao
BongoNewz
Chelsea imekuwa timu ya kwanza kuichapa Arsenal
katika mechi za ligi kuu ya Uingereza msimu huu baada ya kuwachapa 1-2
katika uwanja wao wa nyumbani, Emirates siku ya leo Jumamosi.
Vijana wa Roberto Di Matteo ndio walikuwa wa
kwanza kufunga katika dakika ya 20 kupitia mshambulizi Fernando Torres
baada ya mkwaju wa adhabu kupigwa na Juan Mata.
Lakini katika dakika ya 42
mshambulizi Gervinho alifunga bao safi hivyo kuzifanya timu hizo mbili
ziende mapumzikoni zikiwa sare ya 1-1. Na katika dakika ya 52 ya kipindi cha pili, Mata
alipiga mkwaju mwengine wa adhabu ambapo ulimshinda mlinzi Laurent
Koscielny na badala yake kumgonga mguu na kuingia ndani huku ikimuacha
Kiper wa Arsenal Vito Mannone hoi. Wenger amekua akilalamika kwamba safu yake ya nyuma imekuwa ikizembea katika mipira ya adhabu.
Licha ya kufungwa huko, Arsenal walitawala ngoma
hiyo nzima ya Jumamosi lakini safu ya mbele ya vijana hao wa Arsene
Wenger iliyonekana kukosa makali na kuwa na kukosa umakini.
0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII