Kwa nguvu hii ya CHADEMA, Mwalimu Nyerere leo angekuwa HAI, angeendelea kukumbatia KADI ya CCM?

Nguvu ya mabadiliko inayoongozwa na chama kilicho moyoni mwa wazalendo wa kweli wa nchi hii inanipa hofu kuamini kama mzee wangu Mwalimu Julius K. Nyerere LEO hii angekuwa hai angeendelea kumiliki kadi ya kisiasa ya kijani yenye alama ya JEMBE na NYUNDO.

Alama hizo muhimu katika historia na siasa za nchi hii, zilikuwa ni uashirio wa mambo makuu mawili, JEMBE= Mkulima, NYUNDO=Mfanyakazi. Lakini leo ni kinyume kabisa tena kabisa, JEMBE = Vyombo vya Dola, NYUNDO = Risasi/mabomu.

Hali ya kisiasa ndani ya ccm imekuwa ya mikingamo, huku wimbi la ufisadi nchini likishamiri kila uchao, hata wale wahafidhina wa chama wamegeuka kuwa wakwasi wa chama hiki mufilisi. Sasa hivi dhana ya kuitwa chama cha siasa imetoweka na sasa kinajieleza bila kuuliza kuwa ni GENGE la walanguzi wa raslimali za umma.

Kupitia chama hiki, watu wanafanya jambo lolote watakalo, hata wakiitaka roho yako leo hii wanapata tu. Wameweza kupakia twiga kwenye ndege, wameweza kuza madini, wamehongwa suti, wamehonga vyeo nyumba ndogo, wamejiuzia migodi, wamejipa tenda.

Yani ukiwa ccm hakuna unalolishindwa, wanafikiria kama kuna japo hata uwezekano wa kuitoa roho ya Mtume s.w au Yesu Kristu ilimradi kuondoa dhana ya dhambi kwako.

Nikiangalia utawala wa Mwalimu Nyerere najiona mimi nimkosaji mkubwa ninaestahili adhabu mbele ya ghadhabu ya mungu, kwanini haya yanatokea huku watanzania tukiacha hawa mumiani waendelee kuliangamiza taifa?

Rais wa kwanza Mwl. Nyerere pamoja na kutokuwepo rasilimali nyingi wakati huo alijenga kiwanda karibia kila mkoa. Alijenga nyumba za serikali ambazo wezi Mkapa na Magufuli wamekuja kuuza, alijenga bandari Dar, Tanga, Mtwara, Mwanza, ALIONGOZA SERIKALI YENYE NIDHAMU AMBAYO RUSHWA ILIKUWA NI MWIKO. Alileta umoja wa kitaifa kwa kuongoza serikali bila kujali dini wala. Wakati wake elimu ilikuwa inatolewa bure tena kwa ubora wa hali ya juu. Wakati wake shule zilikuwa na vifaa na waalimu. Wakati wa Kikwete elimu katika shule za msingi na sekondari imekuwa na mzaha tu. Si hayo tu bali mwalimu alijenga nidhamu ya chama, kiasi kwamba kila mtanzania alijivunia kuitwa mwanaccm.

Ikumbukwe kuwa enzi hizo taifa lilikuwa likitegemea pamba, mkonge na tumbaku tu kujipatia fedha za kigeni, lakini kwa hekima za viongozi wa enzi hizo chini ya Mwalimu, waliwahudumia watanzia bila mawaa.

Hivi leo mwalimu angekuwepo, angeendelea kukumbatia kadi ya ccm?

SOURCE: JF
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII

Copyright © 2013. ArtAfropixels Media.com - All Rights Reserved
Customized by: IT XPERTTZ ONE | Powered by: BS
Designed by: Tilabs