Nisha: "Mimi na Nay wa Mitego Tutaoana Muda Wowote"

SALMA Jabu ‘Nisha’ ambaye ni msanii wa tasnia ya filamu Bongo, ameibuka na kunadi uhusiano wake na msanii wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ kwamba mambo yamekwiva na muda wowote atavutwa ndani.

Nisha aliyasema hayo alipokuwa akiongea na Gladness Malya wa GPL...Alifunguka hivi: “Mimi na Nay wangu sasa mambo safi. Muda wowote mnaweza kusikia mengine. Mama yangu amemkubali na amempokea kwa mikono miwili. Kikubwa alikuwa hataki kusikia natoka na mume wa mtu.

“Ameridhia kwani hachagui kabila wala dini ilimradi awe siyo mume wa mtu. Kwa sasa Nay yupo kwenye shoo za Fiesta, akimaliza tutaanza taratibu za ndoa.”
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII

Copyright © 2013. ArtAfropixels Media.com - All Rights Reserved
Customized by: IT XPERTTZ ONE | Powered by: BS
Designed by: Tilabs