ROBBY ONE & BIG JAHMAN WAPELEKWA JELA KWA MALI YA WIZI.....

BongoNewz
Mmiliki wa maduka ya Robby One Fashion, Maarufu kama Robby One pamoja na Big Jahman ambae pia ni mmiliki wa Maduka ya Jahman Fashion, inadaiwa kuwa asubuhi ya leo tarehe 20/09/2012 walipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa tuhuma za kukamatwa na mali za wizi... kikitutaarifu chanzo chetu cha habari hii kilituambia kuwa wajasilia mali hao walikutwa na mizigo ya nguo Kwenye Maduka yao ikiwemo Suti na Viatu aina ya Moka au maarufu kama 4'EnGo ambavyo vinadaiwa kuwa vimeibiwa...Vitu hivyo inasemekena kuwa vina thamani isiyopungua Shilingi Millioni Mia mbili,hivyo kupelekea dhamana ya kesi hio kuwa ni hati ya nyumba kwa kila mtuhumiwa, chanzo chetu kinasema kuwa Wadau hao hawakuweza kutimiza ama kuwasilisha Hati hizo za nyumba ili kupata dhamana, hivyo kupelekea Moja kwa moja kupandishwa kwenye Kalandinga na kupelekwa Segerea
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII

Copyright © 2013. ArtAfropixels Media.com - All Rights Reserved
Customized by: IT XPERTTZ ONE | Powered by: BS
Designed by: Tilabs